1.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (mwenye
suti ya bluu) akiwaeleza jambo wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya
Ihungo ya Kagera, alipofanya ziara hivi karibuni. Kulia (mwenye suti ya udongo
ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bw. Philip Boniventura.
·Aridhishwa na Ujenzi wa Ihungo Boys
Na
Mwandishi Wetu, Bukoba
WAKATI
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe ameomba
taasisi za serikali, Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wizara, ambazo zimeipa
kazi Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania (TBA), kuwa na subira kwa kuwa inaupungufu
wa wafanyakazi, lakini ameridhishwa na ujenzi wa shule ya sekondari ya Wavulana
ya Ihungo ya mkoani Kagera iliyojengwa na taasisi hiyo.
Akifafanua
Mhe. Kamwelwe amesema TBA wanakumbwa na changamoto kubwa ya upungufu wa
wafanyakazi, ambapo kwa Tanzania nzima wanawafanyakazi 300 pekee, ambao
wanajitoa kwa kufanya kazi kwa bidii, ambapo idadi kamili inayotakiwa ni
wafanyakazi 1,700.
1.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo ya
Serikali Tanzania (TBA) mkoa wa Kagera, Mhandisi Herico Bahati (mwenye shati la
batiki) akimpa maelezo mbalimbali Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Isack Kamwelwe (kushoto) kuhusiana na ujenzi wa shule ya sekondari ya
wavulana ya Ihungo, waliyoijenga baada ya awali kuharibiwa na tetemeko la ardhi
lililotokea mwaka 2016. Mbele ni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Philip
Boniventura.
Hatahivyo, ameipongeza TBA kwa kufanya kazi nzuri za ujenzi wa majengo mbalimbali ya serikali kwa kutumia thamani halisi ya fedha, tofauti na wakandarasi binafsi, ambao wamekuwa na gharama kubwa.
“Utendaji
wa TBA bado unaleta mashaka nchi nzima na nimefanya nao kikao nikabaini wapo
wafanyakazi 300 pekee na wanatakiwa angalau 1000 ili waweze kufanya kazi kwa
ufanisi zaidi, hivyo nashauri pamoja na kusikia malalamiko kila upande kutoka
kwa Wakuu wa Wilaya, Mikoa, Bungeni na Watendaji wengine wa serikali,
ninayafanyia kazi likiwemo la uhaba wa wafanyakazi,” amesema Mhe. Kamwelwe.
Baadhi
ya kazi za ujenzi wanazofanya na walizofanya TBA ni pamoja na ujenzi wa Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma mkoani Dodoma; ujenzi wa hospital ya
Mkoa wa Simiyu na Ujenzi wa nyumba za watumishi wa umma mikoa mbalimbali.
Akizungumzia
ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya Katika hatua nyingine, Mhe.
Kamwelwe ameipongeza TBA kwa ujenzi wa shule ya kisasa ya sekondari ya wanaume
ya Ihungo iliyoathirika na tetemeko la ardhi lililotokea Kagera 2016.
“Nawapongeza
sana kwa kujenga shule nzuri tena kwa gharama nafuu ya Bil. 10.4, ukiangalia
wengine walitaka kujenga kwa Bil. 36, hivyo TBA wameokoa fedha nyingi sana za
Watanzania na kiwango chao cha kazi ni kizuri,” amesema Mhe. Kamwelwe.
1.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya
Wavulana ya Ihungo na wa shule ya sekondari Bukoba, wakinawa mikono katika
mabomba ya kisasa, ambayo yamejengwa na Wakala wa Majengo ya Serikali Tanzania
(TBA) baada ya shule hiyo kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka
2016.
Naye
Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Kagera, Mhandisi Herico Bahati amesema ujenzi wa
shule hiyo ulianza Oktoba 5, 2016, ambapo kuna majengo matatu ya ghorofa ya
madarasa yenye vyumba 24, ofisi 12 za walimu, jengo la vyoo 80, mabweni matatu
yenye vyumba 96, nyumba 30 za walimu, upanuzi wa bwalo la chakula na wamechimba
kisima cha maji.
Shule
hiyo inawanafunzi 600, ambapo sasa pia imeongezewa wanafunzi 751 wa shule ya
Sekondari ya Bukoba waliohamishiwa hapo kwa muda baada ya shule yao kuezuliwa
paa na upepo mkali uliotokea Oktoba 2018.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Muleba, ambaye pia anakaimu wilaya ya Bukoba
Mjini, Mhandisi Richard Ruyangu ameishukuru serikali kwa kuijenga tena shule
hiyo na sasa wanafunzi wanaendelea na masomo.
“Tunaishukuru
serikali ya Awamu ya Tano ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli kwa kutujengea tena
shule nzuri na tunaimani kwa mazingira haya watoto watasoma kwa bidii, na hata
walimu hali kadhalika watafundisha kwa moyo tumeona wamejengewa nyumba nzuri na
za kisasa tena zipo maeneo ya karibu na shule itakuwa hawatoki mbali kuja
kufundisha,” amesema Mhandisi Ruyangu.
1.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya
wavulana ya Ihungo wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe wakati alipotembelea shule hiyo kukagua
maendeleo ya ujenzi wake. Shule hiyo imejengwa na Wakala wa Majengo ya Serikali
Tanzania (TBA) baada ya kuharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mwaka 2016.
Kiranja
mkuu wa shule hiyo, Athuman Mohamed kwa niaba ya wanafunzi wenzake,
ameishukuru serikali kwa kuwajengea tena shule yao na wameahidi kusoma kwa bidi
ili kufanya vizuri katika masomo yao
.
.
No comments:
Post a Comment