|
Wachezaji wa Yanga, Mrisho Ngassa (kushoto), Kaseke na Ibrahim Ajibu wakifurahia moja ya mabao yao katika Ligi kuu Tanzania Bara.
|
Na Mwandishi Wetu, Bukoba
KASI ya mabingwa wazamani wa soka Tanzania Bara, Yanga imezidi kuwatia hofu baada ya kuendeleza ushindi katika mechi za ugenini kwa kuifunga Kagera Sugar kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa kaitaba mjini hapa.
Yanga wiki iliyopita ilianza mechi za ugenini kwa ushindi kama huo dhidi ya Mwadui ya Shinyanga katika mchezo mwingine wa ligi hiyo uliofanyika kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Wadau wengi wa soka zikiwemo Simba na Azam, walitegemea kuwa Yanga itakapoanza kucheza mechi za ugenini itapunguzwa kasi yake katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini timu hiyo imeonekana kutopoa na kuendeleza makali yake hata ugenini.
Huo ni ushindi wa pili wa
Yanga ugenini na Kanda ya Ziwa baada ya wiki wili iliyopita kuibuka na ushindi
kama huo dhidi ya Mwadui ya Shinyanga katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja
wa Kambarage.
Ushindi huo wa jana
uliopatikana kupitia kwa wachezaji wake, Heritier Makambo
na Raphael Daud yalitosha kabisha kuiwezesha Yanga kuibuka na ushindi huo na kuondoka na pointi zote tatu na kufikisha pointi
32, moja nyuma ya vinara Azam FC baada ya kucheza mechi 12 sawa na watani zao
Simba waliopo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 27.
Makambo aliandika bao la
kwanza katika dakika ya 21 kwa kichwa akipokea pasi kutoka kwa Haji Mwinyi huku
lile la kusawazisha la Kagera Sugar likiwekwa kimiani na Ramadhani Kapera.
Penalti hiyo ilitolewa na
mwamuzi baada ya kipa wa Yanga kumchezea vibaya Jacob Ningo aliyekuwa akijaribu
kufunga.
Yanga ilijihakikishia
ushindi katika dakika ya 74 kwa bao la Daud, ambaye alijaza mpira kwa kichwa
baada ya Pango Godfrey kupiga mpira uliomkuta mchezaji mmoja wa Yanga aliyepiga
mpira kwa kichwa uliomkuta mfungaji aliyeujaza kimiani.
Yanga imehitimisha viporo
vyake vizuri baada ya kushinda mchezo huo wa jana ugenini wakati ikielekea
kukamilika duru la kwanza.
Msimamo
P W D L GF GA +/- Pts
Azam 13 10 3 0 17 3 14 33
Yanga 12 10 2 0 21 6 15 32
Simba 12 8 3 1 23 4 19 27
Mtibwa 14 7 2 5 17 11 6 23
Coastal 14 5 7 2 11 9 2 22
JKT Tanzania 13 4 7 2 7 6 1 19
Mbeya City 14 5 4 5 15 16 -1 19
Mbao 13 5 4 4 10 11 -1 19
Singida United 14 5 3 6 12 14 -2 18
Kagera Sugar 14 3 8 3 11 11 0 17
KMC 13 3 7 3 10 7 3 16
Ruvu Shooting 14 4 4 6 13 21 -8 16
Stand United 14 4 2 8 14 21 -7 14
Lipuli 14 2 7 5 7 10 -3 13
Mwadui 14 3 4 7 9 13 -4 13
Ndanda 14 3 4 7 9 20 -11 13
Alliance 14 3 4 7 8 19 -11 13
African Lyon 13 2 5 6 9 13 -4 11
Tanzania 14 1 7 6 7 11 -4 10
Biashara United 13 1 7 5 5 9 -4 10
No comments:
Post a Comment