Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria akizungumza jijini Dar es Salaam leo. |
KATIKA msimu huu wa sikukuu ambapo watu wengi
hujumuika na familia zao kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka, MultiChoice Tanzania
imetangaza ofa kabambe kwa wateja wake na wale wanaojiunga na huduma za DStv
kupitia kampeni yake maalum ijulikanayo kama ‘Ni Muda wa Kukiwasha na DStv’.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo,
Meneja Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria amesema wateja wa DStv sasa
watapata burudani zaidi za kusisimua kupitia Soka, Filamu, Tamthilia, Katuni na
vipindi mbali mbali vya watoto vitakavyoileta familia pamoja na kuimarisha
upendo.
Msanii wa kujitegemea, Omary Mkali akitumbuiza wakati wa hafla ya Mult-choice leo. |
Kwa mujibu wa Alpha, zaidi ya maudhui hayo yote
yaliyotajwa hapo juu; Katika kunogesha sikukuu, maudhui mapya yatayoongezwa
ndani ya DStv.
Maudhui hayo ni pamoja na tamthilia ya Kapuni ambayo inaingia
msimu wake wa pili katika chaneli ya Maisha Magic Bongo (MMB), Chaneli maalum
(EA Movies) yenye mkusanyiko wa filamu bora za Afrika Mashariki, na pia sinema
maalum za watoto katika chaneli ya Mnet inayojulikana kama Mnet ANIMANIA pamoja
na vipindi mbalimbali vinavyohusiana na msimu huu wa sikukuu.
Aidha, Alpha
alisisitiza kuwa, Kipindi hiki cha sikukuu kupitia chaneli ya Maisha Magic
Bongo (MMB) itawaletea wateja maudhui mapya na ya kusisimua zaidi, hivyo
kuwasihi watanzania wakae tayari kupokea kitu kipya kutoka MMB tarehe 14
Disemba 2018.
Mkuu wa Mauzo wa kampuni hiyo Salum Salum akizungumza leo. |
Kwa wateja wapya wanaojiunga na DStv msimu huu
watapata ofa maalum ya kuunganishwa kwa shilingi 79,000 pamoja na zawadi maalum
ya kifurushi cha mwezi cha Bomba bila malipo ya ziada. Ofa hii itaendelea kwa
muda wa miezi miwili kuanzia tarehe 15 Novemba 2018 na ni kwa nchi nzima.
Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Omary Kopa. |
“Mbali na kuongezwa kwa chaneli na maudhui kedekede
kwa wateja walipo wa DStv, pia kwa wale ambao bado hawajajiunga hatujawasahau,
sasa tunawapa ofa hiii kabambe ya kujiunga kwa gharama nafuu na zaidi ya hapo
wapate kifurushi cha mwezi mmoja bila malipo. Hii ni zawadi yetu ya sikukuu kwa
wateja wetu” alisema Salum Salum.
Johnson Mshana na Shumbana wakati wa hafla hiyo leo. |
Amesisitiza kuwa ofa hii ni kwa nchi nzima na tayari
wameshajipanga na mawakala wote kuhakikisha kuwa ofa hii inapatikana nchi
nzima. “Mtu yeyote asiwe na wasiwasi wa jinsi ya kuunganishwa kwa ofa hii.
Tunao mawakala wetu wa usambazaji na ufundi nchi nzima, hivyo hata walio maeneo
ya vijijini huduma hii watapata.
Wakati huohuo, DStv leo imewakabidhi waandishi wa habari zawadi za ving'amuzi na dishi na kuahidi kuwafungia vifaa hivyo baada ya kujibu maswali vizuri kuhusu 'Ni Muda wa Kukiwasha na DStv’.
No comments:
Post a Comment