PARIS, Ufaransa
KOCHA wa timu ya Paris Saint-Germain (PSG), Thomas
Tuchel amesema kuwa washambuliaji wake nyota wawili, Neymar na Kylian Mbappe watakuwa
tayari kwa ajili ya kukabili Liverpool katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa
Ulaya.
Wawili hao waliumia wakati wakizichezea tiu zao za
taifa na walikosa mchezo wa PSG, ambayo ilishinda bao 1-0 dhidi ya Toulouse
lakini Tuchel alisema kuwa ana matumaini wachezaji hao wawili watakuwemo katika
kikosi cha PSG kesho Jumatano.
"Wanaendelea vizuri siku hadi siku, tuna muda
kabla ya Jumatano. Ni jambo zuri kwetu. Nafiiri wataweza kucheza, “alisema
Mjerumani huyo katika mahojiano katika kipindi cha televisheni cha Telefoot.
PSG wana pointi tano baada ya raundi nne za mechi za
Ligi ya Mabingwa wa Ulaya hatua ya makundi na ushindi wa mchezo huo wa katikati
ya wiki kwa kocha Jurgen Klopp na ule wa Napoli iliyopo katika nafasi ya pili,
utawaondoa mabingwa hao wa Ufaransa katika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza
tangu waliporejea katika mashindano makubwa Ulaya mwaka 2012.
--
Wakati
huohuo, mabingwa wa England Manchester City leo Jumanne
wanaifuata Lyon ya Ufaransa katika mchezo mwingine wa Ligi ya Mabingwa wa
Ulaya.
Man City ilihitaji kuvunja benki na kutumia kiasi cha
pauni milioni 80 kwa ajili ya kuwasajili John Stones na Nicolas Otamendi wakati
nahodha wake Vincent Kompany akirejea katika ufiti baada ya kuwa majeruhi kwa
muda.
Wakati akirejea kutoka Athletic Bilbao, Laporte alitumia
muda kuzoea mazingira katika mechi tatu walizocheza nje ya uwanja wa nyumbani
zikishia kwa vipigo wakati wakimaliza msimu.
No comments:
Post a Comment