Na Mwandishi Wetu, Hai
WAKENYA wametamba
katika mbio za kwanza za Kilimanjaro International Airport Marathon 2017 baada
ya kushika nafasi za juu katika kilometa 21 na 42 kwa wanaume na wanawake.
Ushindi huo
umefanya mamilioni ya fedha za zawadi kwenda nchini Kenya baada ya Duncan
Kwemboi kushika nafasi ya kwanza katika mbio za kilometa 42 kwa kutumia saa
2:19:10 na Meshack Kirotich kumaliza wa pili kwa kutumia saa 2:21:25.
Mshindi wa tatu
katika mbio hizo za marathon naye alikuwa Mkenya, Abraham Too aliyemaliza kwa
kutumia saa 2:22:42.
Katika mbio za
kilometa 42, ambazo mshindi wa kwanza hadi watatu aliondoka na Sh milioni 5, milioni
4 na milioni 3.
Kwa upande wa
wanawake, katika kilometa 42 mbio hizo nazo zilitawaliwa na Wakenya,huku
Failuna Abdi ndiye alikuwa Mtanzania aliyeshika nafasi ya juu baada ya kumaliza
watatu katika mbio za kilometa 21.
Failuna alimaliza
mbio hizo kwa kutumia saa 1:16:22 na kujinyakulia kiasi cha sh milioni 2, huku
Dickson Marwa naye wa Tanzania alimaliza watano katika kilometa 21 kwa wanaume.
Marwa ambaye hivi
karibuni alitamba katika mbio za Rock City Marathon na zile za Zanzibar, wakati
katika mbio za KIA alipata sh milioni 1.5 baada ya kutumia saa 01:06:51.
Abdi akizungumza
baada ya kumaliza mbio hizo alisema kuwa anasikitika sana kwa Wakenya kutawala
mbio hizo kwani Watanzania kama wangejiandaa vizuri wangeweza kushinda.
Aliwataka
wanariadha wa Tanzania kufanya mazoezi kwa bidii ili kuhakikisha wanafanya
vizuri katika mbio zingine ndani na nje ya nchi.
Naye Marwa
alisema kuwa ushindi ulikuwa mkali hasa kutoka kwa Wakenya ambao walikuwa wengi
katika mbio hizo, lakini amefarijika kuwa Mtanzania aliyemaliza katika nafasi
ya tano.
Mshindi wa mbio
za kilometa 21 kwa wanaume, Mkenya Joel Kipmatai alisema kuwa mbio zilikuwa
nzuri lakini hawakupata upinzani mkubwa kutoka kwa Watanzania.
Alisema mbio hizo
zimeanza vizuri na zinatakiwa kurekebisha matatizo machache ili kuzidi
kuziboresha na kuwa moja yam bio kubwa duniani miaka ijayo.
Mgeni rasmi
katika mbio hizo za Kwanza za Kilimanjaro Internatinal Airport alikuwa Naibu
Spika wa Bunge, Dk Tulia Nackson aliyekabidhi zawadi kwa washindi.
No comments:
Post a Comment