Na
Mwandishi Wetu
MAMLAKA
ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imesema itahakikisha inapata hati za
viwanja vyake vya ndege ili kupunguza uvamizi kutoka kwa wananchi.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Bw. Richard Mayongela
alitoa kauli hiyo leo kwenye mkutano na wafanyakazi uliofanyika katika
ukumbi ya Transit uliopo jengo la Kwanza la abiria la Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI), ikiwa ni moja ya mikakati ya mamlaka
hadi kufikia Juni 2018.
Bw.
Mayongela alisema tayari wameanza taratibu za kupata hati miliki kwa viwanja
13, vikiwemo vya JNIA na Mwanza zilizofutwa awali.
Hata
hivyo, Wananchi wamekuwa na tabia za kuvamia maeneo ya viwanja vya ndege kwa
kufanya makazi na mashamba, jambo ambalo ni hatarishi kiusalama.
Bw.
Mayongela alisema mkakati mwingine ni kushirikiana na Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ), kuimarisha ulinzi kwenye maeneo ya viwanja vya ndege 58 vinavyomilikiwa
na serikali na ambavyo havipo chini ya serikali.
“Pia
tutaanda kikosi kazi kitachosaidiana na wenzetu wa TANROADS katika usimamizi na
uangalizi wa viwanja vya ndege vinavyoendelea
kujengwa maeneo mbalimbali nchini,” alisema Bw. Mayongela.
Katika
hatua nyingine Bw. Mayongela alisema pia mamlaka inampango wa kuendeleza
miundombinu mbalimbali yakiwemo majengo ya abiria, Mizigo, ufungaji wa taa za
kuongezea ndege na ufungaji kamera za usalama (CCTV) kwenye viwanja vya Arusha,
Mwanza, JNIA na Dodoma.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Lawrence Thobias aliwataka
wafanyakazi kufanya kazi kwa uweledi na uwazi, ili kufikia malengo yaliyowekwa
na hatakuwa tayari kumfukuza mtumishi kazi kwa masuala yasiyokuwa na msingi.
“Ninafungua
milango kwa wafanyakazi mje ofisini kwangu kwani hii ni ofisi ya rasilimali
watu na sio rasilimali mtu, naweka milango wazi mje tujadili masuala ya kazi ya
kujenga na sio majungu,” alisisitiza Bw. Thobias.
No comments:
Post a Comment