Sunday, 5 November 2017
Wydad mabingwa wapya Ligi ya Mabingwa Afrika
CASABLANCA,
Morocco
TIMU ya Wydad
Casablanca (pichani) imetwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa wa Afrika baada ya kuifunga timu
ngumu ya Al Ahly kwa bao 1-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Stade
Mohamed V Stadium mjini hapa.
Wydad imetwaa taji
hilo baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao 2-1 kufuatia timu hizo kutoka
sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Misri wiki
iliyopita.
Mchezo huo wa pili
wa fainali ulimuliwa kwa bao la Walid El Karti katikati ya kipindi cha pili,
wakati timu hiyo ya Morocco ikitwaa taji lake la pili la Afrika tangu mwaka
1992.
Al Ahly
walionekana kuwa hatari zaidi katika dakika 20 za mwanzo na walipata nafasi
nzuri ya kufunga mwanzoni mwa mchezo wakati Abdallah El-Said, alipomjaribu kipa
wa Wydad Zouhair Laaroubi.
Wydad walipambana
na kujaribu kuweka pamoja mashambulizi yao na katika dakika ya 30, mshambuliaji
Abdeladim Khadrouf nusura afunge baada ya shuti lake mgonga beki na kugonga
mwamba.
Ahly baada ya
dakika kadhaa walikosa bao baada ya kufanya shambulizi la nguvu, ambapo Moemen
Zakareya alipata nafasi nzuri lakini iliokolewa na Laaroubi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment