Wanariadha wakichuana katika mbio za meta 5,000 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo. |
MKOA wa Arusha umekuwa bingwa wa kwanza wa
mashindano ya taifa ya riadha yaliyomalizika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam.
Arusha walitawazwa mabingwa baada ya kumaliza
wakiwa na medali mbili za dhahabu. Tatu za fedha na moja ya shaba, huku wenyeji
Dar es Salaam walishika nafasi ya pili kwa kupata medali mbili za dhahabu na
moja ya shaba.
Timu ya mkoa wa Kaskazini Pemba ilitwaa
nafasi ya tatu baada ya kupata medali moja ya dhahabu, moja ya fedha na tatu za
shaba.
Katika mashindano hayo yaliyofungwa jana na
Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida nafasi ya nne ilikwenda kwa mkoa wa
Kaskazini Unguja iliyopata medali moja ya dhahabu na moja ya fedha.
Pwani walishika nafasi ya tano baada ya
kupata medali moja ya dhahabu na moja ya fedha, huku Tabora wakimaliza wa sita
kwa medali moja ya dhahabu na moja ya fedha.
Dodoma walimaliza wa saba wakiwa na medali
moja ya dhahabu na moja ya shaba huku Kilimanjaro ikimaliza na medali moja ya
dhahabu na kumaliza katika nafasi ya nane.
Kivutio katika ufungaji jana ilikuwa katika
mbio za meta 5,000 wakati mwanariadha wa Mwanza, Silvia Masatu licha ya
kukimbia akiwa peku, alitoka nyuma na kumshinda Amina Mohamed wa Arusha kwa
kutumia dakika 17:52:00.
Mwanariadha wa Mkoa wa Ruvuma, Rose Seif akiruka chini katika mashindano ya taifa ya wanawake leo kwenye Uwanja wa Taifa. |
Amina alimaliza wa pili baada ya kuongoza kwa
muda mrefu na kumaliza mbio hizo kwa dakika 18:03:37 wakati Anastazia Dolimongo
wa Shinyanga alimaliza watatu kwa dakika 18:06:50.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
kwa udhamini JICA, lengo ni kuchagua timu ya taifa itakayosaka viwango vya
kushiriko Olimpiki ya 2020 Tokyo.
Wanariadha wa mchezo wa kuruka chini wakipewa maelekezo kabla ya kushiriki katika mchezo huo leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. |
No comments:
Post a Comment