Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki
Tanzania, TOC, Filbert Bayi (kulia).
|
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) ni miongoni mwa vyama vichache
vya michezo, ambavyo vimeshindwa kuthibitisha ushiriki wake katika Mkutano Mkuu
wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, imeelezwa.
Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa TOC, umepangwa kufanyika mjini Dodoma
Desemba 10 na Novemba 4 ndio ilikuwa mwisho kwa vyama kuthibitisha kushiriki.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi
alisema kuwa TFF na Shirikisho la Mpira wa Kikapu (TBF) vimeshindwa
kuthibitisha kushiriki katika mkutano huo mkuu.
Alisema kuwa vyama au mashirikisho ya michezo inayoshindwa kufuata
taratibu kama hizo za kuthibitisha kushiriki alafu baadae ndio wanavuruga
utaratibu kwa kushiriki bila ya kuthibitisha.
Alisema endapo chama kinathibitisha kushiriki kuna wasaidia TOC kuwapangia
majumbe malazi na taratibu zingine zikiwemo hata kuwaandaalia dokumenti
mbalimbali za katika mkutano.
Aidha, Kamati ya Utendaji ya TOC inatarajia kufanya kikao cha
mwisho kabisa cha Kamati ya Utendaji Desemba 25 Zanzibar kabla ya kufanyika kwa
mkutano mkuu huo wa uchaguzi.
Wakati
huohuo, Kamati ya Uchaguzi ya TOC imeanza kazi ya kupitia fomu za wale
wote wanaotaka kugombea nafasi mbali mbali za uongozi.
No comments:
Post a Comment