Na Mwandishi Wetu
MBIO za tatu za Kilimanjaro
Health Marathon 2016 zitafanyika mjini hapa Desemba 4, imeelezwa.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Moshi, Mkurugenzi wa Community Vission & Better Future, Luka Ndalima
alisema mbio hizo zitakuwa za kilometa
10, 5 na tatu.
Alisema zinatarajia kuanza
na kumalizikia katika viwanja vya Majengo Mjini Moshi.
Ndalima alisema lengo la
mbio hizo za kila mwaka ni kutoa elimu ya afya katika Siku ya Ukimwi Duniani
pamoja na ile ya Walemavu, ambazo zote hufanyika Desemba.
“Siku ya Ukimwi Duniani hufanyika Desemba mosi wakati ile ya
walemavu nayo hufanyika mwezi huo huo, hivyo tumeamua kuzisherehekea pamoja
Desemba 4, wikiendi ya kwanza ya mwezi Desemba," alisema Ndalima.
Alisema kuwa pia mbio hizo
zinatumika kutoa elimu ya afya na kuwataka kutowaficha ndani walemavu na badala
yao wawatoe na kuwapatia elimu kama watoto wengine.
Alisema mafunzo watakayotoa
ni kuwaelimisha watu kuhusu kujikinga na maambukizo mapya ya Ukimwi hasa kwa
upande wa vijana.
Alisema mwaka jana
walishiriki jumla ya wakimbiaji 1,200 huku watu wazima wakiwa 800 na watoto ni
400, ambapo mwaka huu wanatarajia kupata washiriki wengi zaidi.
No comments:
Post a Comment