Mgeni rasmi pamoja na waheshimiwa wengine wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ufunguaji wa uzinduzi. |
MAISHA Magic
Bongo kwa kushirikiana na maprodyusa wa filamu nchini wameleta mapinduzi makubwa kwenye
sanaa ya filamu za Kibongo.
Palikuwa na
full shangwe na vifijo kwenye ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa, Novemba 4,
2016. Shangwe hii ni baada ya Maisha Magic Bongo kwa kushirikiana na
Multichoice Tanzania kuzindua rasmi chaneli yao ya (160) Maisha Magic Bongo.
Miongoni mwa waalikwa walikuwa waigizaji maarufu na maprodyusa wa filamu
nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multchoice-Tanzania, Maharage Chande akizungumza katika hafla hiyo. |
Uzinduzi huu
ulilenga kwenye kusheherekea kazi nzito za maprodyusa wetu wa filamu hapa
nyumbani , na utambulisho rasmi wa chaneli yetu yenye mandhui ya kitanzania.
Chaneli hii imelenga kuburudisha na kuelimisha watazamaji wetu wa kitanzania kupitia
filamu, tamthiliya, na maigizo mbalimbali ya Kiswahili.
Mkurugenzi Mkuu wa MNET, Yalisa Phawe akizungumza. Kulia ni Mkuu wa Chaneli ya Maisha Magic Bongo, Barbara Kambogi. |
Chaneli hii inapatikana
kwenye kifurushi cha huduma za DStv (160). Uzinduzi huo ulifuatiwa na maonesho
ya tamthilia ya kimapenzi ya “Huba”, na vidokezo vya video za mambo yajayo
yaliyoandaliwa kwenye chaneli ya Maisha Magic Bongo. Watazamaji wetu wajiandae
kwa uhondo zaidi kupitia vipindi vijavyo vya “Harusi Yetu”,
Mwenyekiti wa Bodi ya DSTV, Balozi Ami Mpungwe. |
Movi za kihindi
zenye tafsiri ya Kiswahili kama “Doli”, na filamu mbalimbali kuanzia msimo mpya
wa Februari 2017.
Wakati wa
mahojiano na waandishi wa habari, Mkuu wa chaneli ya Maisha Magic Bongo Barbara
Kambogi alisema “Tumefurahia kupata fursa ya kuwapatia watazamaji wetu wa
kitanzania chaneli ya Maisha Magic Bongo yenye mandhari halisi ya Kiswahili.
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fisoo. |
Kwani kwa pamoja tumeweza kuiendeleza
tasnia yetu ya kitanzania. Ndugu zangu, huu ni mwanzo tu wa Maisha Magic Bongo
na tunatarajia kusonga mbele. Tutaendelea kushirikiana na maprodyusa wa filamu
za hapa nyumbani, kwani sasa tumewapa fursa maprodyusa wetu kutusaidia
kuitangaza sanaa yetu ya Tanzania kwenye masoko ya nje.”
Maisha Magic
Bongo chaneli (160) imewaandaliwa mambo mazito na ya uhakika ili
kuburudisha wateja wetu na kujivunia utanzania wetu kupitia kazi
nzito za maprodusa na waigizaji wetu.
Mgeni rasmi
alimalizia kwa kuishukuru Maisha Magic Bongo kwa kuisogeza mbele sanaa ya
filamu ya Tanzania na kuendeleza vipaji vya maprodyusa wetu kupitia kazi zao
nzuri.”
No comments:
Post a Comment