MANCHESTER, England
KOCHA wa Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa kufanya kwake
vizuri katika Ligi ya Mabingwa wa Ulaya haina maana kuwa ana uhakika wa kufanya
vizuri katika mashindano hayo msimu huu.
Katika misimu saba kama kocha wa Barcelona na Bayern Munich, Guardiola mwenye umri wa miaka 45 ameshinda mara tatu taji la Ligi ya Mabingwa na
hajawhi kushindwa kufuzu kwa nusu fainali.
Man City msimu huu imefikia hatua ya mtoano ya mashindano hayo
huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi.
"Wakati wote inaonekana kama rahisi lakini kila kitu ni
kigumu, “alisema Guardiola.
Timu hiyo ya kocha huyo Mhispania itamaliza ya pili katika Kundi
C, ikiwa na maana kuwa wataikwepa Bayern Desemba 12 wakati itakapopangwa ratiba ya hatua ya 16
bora.
Juventus na Borussia Dortmund ni wapinzani wanaotarajia kkutana
pamoja na Monaco, ambao wamemaliza kileleni katika kundi ambalo Tottenham walitolewa
katika mbio hizo.
Man City ilitinga hatua ya nusu fainali msimu uliopita, ambapo
huku nyuma haijawahi kuvuka hatua ya 16 bora.
"Tunazungumza kuhusu Manchester City kucheza hatua ya nusu
fainali lakini kuna timu nzuri kibao Ulaya, “alisema Guardiola.
"Kucheza robo fainali sio jambo la kawaida. Wakati
unapofanikiwa kucheza nusu fainali au fainali, ni kitu kisicho cha kawaida.
"Kiwango chetu sasa ni kucheza hatua ya mtoano kama ni
kiwango chetu cvha chini, ndio miaka sita iliyopita hilo halikuwahi kutokea
kamwe.”
No comments:
Post a Comment