Na Mwandishi Wetu
MAKOCHA wa mchezo wa kuogelea wametakiwa kuzingatia mafunzo ili
kwenda kuuendeleza mchezo huo katika maeneo wanakotoka.
Hayo yameelezwa na Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC, Gulam
Rashid wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku 10 ya maocha wa mchezo wa kuogelea hatua ya ju.
Mratibu wa mafunzo ya kuogelea wa
Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Muharami Mchume akizungumza wakati wa
mafunzo hayo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
|
Kozi hiyo ilifunguliwa juzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
ambapo walimu 30 wanapata mafunzo hayo kutoka kwa mkufunzi kutoka Shirikisho la
Kimataifa la mchezo wa kuogelea (Fina), Joshua Neuloh wa Ujerumani.
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi akizungumza wakati wa mafunzo hayo ya
kuogelea.
|
Rashid aliwataka makocha hao kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania
kujifunza kwa makini na kupeleka ujuzi wao huko watokako ili kuuendeleza mchezo
huo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Ramadhani
Namkoveka alisema washiriki hao wanachukua mafunzo ya juu ya ufundishaji mchezo
huo wa kuogelea.
Washiriki wa mafunzo hayo ni kutoka mikoa ya Dar es Salaam,
Arusha, Zanzibar, Mwanza na Singida.
Neuloh akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo alisema kuwa
yatawasaidia makocha hao kufundisha kitaalam kuogelea.
Naye makamu mwenyekiti wa TSA, Thauriya Diria alishukuru Olympic
Solidarity kupitia Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) kuwapatia mafunzo hayo ya
ngazi ya juu ya kuogelea.
Alisema kuwa washiriki wengi ni walimu watasaidia kuueneza mchezo
huo kuanzia chini kabisa na kusaidia kuenea kwa zaidi mchezo huo hapa nchini.
Mkufunzi wa mafunzo kwa makocha wa uogeleaji, Joshua Neuloh wakati wa
mafunzo hayo.
|
Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi na Makamu mwenyekiti wa Chama cha
Kuogelea (TSA), Thauria Hassan Diria.
No comments:
Post a Comment