Mratibu wa Tamasha la Michezo la Karatu, Meta Petro (kulia) akikagua
washiriki wa mbio za baiskeli kabla hazijaanza.
|
Na Mwandishi Wetu
TAMASHA la Michezo la Karatu mwaka huu litafikia kileleni chake
Desemba 17, imeelezwa.
Mratibu wa tamasha hilo la kila mwaka, Meta Petro alisema jana kwa
njia ya simu kuwa, mashindano ya mchezo wa mpira yatafanyika kwa siku mbili
kuanzia Desemba 12 na 16.
Alisema kuwa timu zitakazofuzu kwa nusu fainali zitacheza Desemba 13
kabla ya kutifuana katika fainali Desemba 15 kwa zile zitakazopenya hatua
iliyotangulia.
Petro alisema kuwa fainali ya mchezo wa mpira wa wavu itakuwa
Desemba 16 huku fainali za riadha, mbio za baiskeli zikifanyika Desemba 17 siku
ya ufungaji wa mashindano hayo.
Alisema mwaka huu tamasha hilo linatarajia kuwa kubwa na lenye
msisimko na wakitarajia wachezaji kutoka mikoa mbalimbali watashiriki.
Mbali na michezo hiyo ya soka, riadha, baiskeli na wavu, pia
tamasha hilo hushirikisha ngoma za asili pamoja na nyimbo na sarakasi.
No comments:
Post a Comment