MKUU wa mkoa wa Mwanza John Mongela akiwapongeza wachezaji wa Kilimanjaro Queens walipowasili jijini Mwanza leo kabla ya kupanda ndege kwenda Dar es Salaam. |
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MKUU wa mkoa wa Mwanza John Mongela
ameipongeza timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania Bara, The Kilmanjaro Queens baada ya kuchukua ubingwa wa michuano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) iliyomalizika Jinja, Uganda hivi karibuni.
Timu hiyo ilitwaa ubingwa wa mashindano hayo ya kwanza ya wanawake kuandaliwa na Cecafa baada ya kuifunga timu
ya soka ya Kenya kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini
Jinja, Uganda.
Katika mapokezi hayo ya timu timu hiyo mkoani
hapa,Mongela alizawadia timu hiyo shilingi milioni 1 kama pongezi.
Mongela
amepongeza pia Chama cha Soka cha Wanawake(Twfa) kwa juhudi zao mpaka timu hiyo
imechukua ubingwa.
Mongela ameiomba timu hiyo ihakikishe
inafanya juhudi kuhakikisha wanaendelea kuwa mabingwa. Mwenyekiti wa soka la
wanawake nchini(TWFA) Amina Karuma ameomba makampuni yaendelee kujitokeza katika
kudhamini soka la wanawake.
Karuma pia amepongeza kampuni ya Airtel na
Azam kwa juhudi zao za kusaidia timu hiyo wakati ilipokuwa Uganda.
Karuma amesema ushindi huo umetokana na
matunda ya michuano ya Airtel Rising Star, ambapo wameweza kupata wachezaji.
Kwa
upande wake kocha mkuu wa timu hiyo Sebastian Mkomwa amesema michuano hiyo
ilikuwa migumu sana kwa kuwa waliohofia timu za Kenya na Ethiopia kutokana
zimecheza michuano ya Afcon kwa wanawake.
"Mashindano yalikuwa magumu sana
kutokana na tumefanya mazoezi ya zima moto tulijiandaa wiki moja kabla ya
mashindano,kingine kilichotugharimu ni urefu wa safari kutoka Dar-es-salaam
mpaka Jinja kwa bus".
Mkomwa ameomba wachezaji wawe wanaingia kambini
mapema sana ili kujianda mapema katika mashindano yoyote yale.
Nahodha wa timu hiyo,Sophia Mwasikili
ameiomba Serikali iwekeze zaidi katika soka la wanawake hiyo itasaidia soka la
wanawake kufanya vizuri.
Mwasikili amesistiza wachezaji wawe
wanajaliwa zaidi katika kupewa posho zao na mishahara kwa wakati italeta
motisha kwa wao kufanya vyema.
Mfungaji kutokea timu hiyo,Mwanahamisi
Omary'Gaucho' ambae amefunga magoli matatu amesema yeye aliweka malengo ni
lazima ahakikishe kila mechi anafunga ili kusaidia timu yetu kufanya vyema.
Wachezaji wa Kilimanjaro queens waliofunga
magoli ni Asha Rashid magoli matatu,Donasia Donald mawili, Stumai Rajab magoli
mawili.
Wachezaji walioshinda ubingwa huo ni Fatuma Omary,Sophia Mwakisili,Anastazia Anthony,Fatuma
Issa,Fadhila Hamad,Donisia Donald,Happy Hezron na Asha Rashid.
Wengine ni Wema Richard,Mwanahamisi
Omari,Maimuna Hamis,Fatuma Hassan,Amina Ally,Sherida Boniface,Anna Hebron,Najat
Abass na Fatuma Bashir.
No comments:
Post a Comment