Baadhi ya watazamaji wakifuatilia mashindano ya Shimiwi yaliyofanyika mkoani Morogoro kwenye Uwanja wa Jamhuri. |
Na Mwandishi Wetu
BONANZA la uzinduzi wa Michezo ya Watumishi wa Serikali (Shimiwi),
litafanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, imeelezwa.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Shimiwi Moshi Makuka, bonanza
hilo linatarajia kuanza saa 12:30 asubuhi na kushirikisha watumishi wote wa
Serikali kutoka katika Wizara, Idara zinazojitegemea, Wakala wa Serikali na
Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema kuwa mgeni rasmi katika bonanza hilo atakuwa Katibu Mkuu
Kiongozi na Mkuu wa Watumishi wa Umma Balozi John Kijazi.
Michezo ya mwaka huu ya Shimiwi itafanyika mkoani Dodoma kuanzia
Oktoba 14 hadi 27.
Makuka alizitaja sababu zilizopelekea kufanyia michezo hiyo mkoani
Dodoma ni pamoja na kuunga mkono agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli la
Serikali kuhamia katika Makao Makuu Dodoma.
Sababu nyingine ni kuwapa nafasi Watumishi wa Umma ambao
hawajawahi kufika Dodoma kufahamu mazingira na kufanya maandalizi muhimu kwa
ajili ya kuhamia.
“Tarehe 14 Oktoba, 1999 siku
ambayo Mwalimu Nyerere alipoaga Dunia Watumishi wa Umma tulikuwa katika michezo
hii mkoani Morogoro, hivyo sisi (Watumishi wa Umma) tahrehe hiyo ni kumbukumbu
muhimu ya kifo chake, pia ni ni kuenzi agizo lake la kuhamia Dodoma…, “alisema
Makuka.
Alisema kuwa michezo ya mwaka huu itaanza kwa ibada maalum kwa
ajili ya kumuombea Baba wa Taifa pia kumtakia afya njema Rais Magufuli pamoja
na wasaidizi wake.
Pia Shimiwi itatumika kupanda miti katika maeneo yatakayoelekezwa
na Serikali ya mkoa wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment