LONDON, England
BINGWA wa Olimpiki wa mbio za meta 5,000 na 10,000 Mo Farah alijikuta
katika wakati mgumu baada ya kubaguliwa na mfanyakazi wa ndege na kurudisha
nyuma katika mstari kabla ya kupanda ndege kwenda Marekani, alisema mke wake.
Tania Farah alisema mfanyakazi wa Shirika la Ndege la Delta alimtilia
ngumu bingwa huyo mara nne wa medali za dhahabu za Olimpiki na kugoma kabisa
kuamini kama mwanariadha huyo ana tiketi ya daraja la pili (business class).
Hatahivyo, taarifa zingine zilisema kuwa Farah na familia yake
hiyo walichelewa kupanda ndege wakati abiria wa daraja la kwanza walipokuwa
wakiingia katika ndege.
Msemaji wa Delta Airlines alisema baadae kuwa wanachunguza madai
hayo na "watalifanyia kazi moja kwa moja kwa kushirikiana na familia hiyo
ya Farah".
Tukio hilo inadaiwa lilitokea Agosti 22 wakati wawili hao pamoja
na watoto wao wanne wakirejea kutoka katika Olimpiki ya Rio 2016, ambako Farah alitetea
mataji yake yam bio za meta 5,000 na 10,000.
Farah na familia yake walikuwa katika hatua za mwisho za safari
yao kutoka Atlanta kurudi kwao Portland, Oregon.
"Najua alikuwa na tatizo na yeye, “alisema.Tania Farah katika gazeti la Jumapili la Telegraph, akimnukuu
mfnayakazi huyo wa Delta Airlines.
"Huyu manamke alimdharirisha hadi watu walipokuja na kusema:
'Huyi ni Mo Farah, ni bingwa wa Olimpiki,”alisema mke
wake.
Farah, 33, alitarajia kuwa mtu wa kwanza kushinda mara tatu
mfululizo mbio za Great North Run wakati wa mbio hizo Newcastle leo Jumapili.
No comments:
Post a Comment