Baadhi ya wachezaji wa timu ya taifa ya Hispania wakishangilia moja ya mabao yao dhidi ya Liechtenstein. |
HISPANIA imetoa onyo kwa timu zinazoshiriki
katika kinyang’anyiro
chakusaka tiketi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi
baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 8-0 dhidi ya Liechtenstein.
Mabao yao saba yalipatikana katika kipindi
cha pili wakati Liechtenstein wakijaribu kupambana baada ya kuwapelekesha
wenyeji wao mwanzoni mwa mchezo.
Diego Costa, David Silva na Alvaro Morata wote
kila mmoja alifunga mara mbili wakati Sergi Roberto na Vitolo nao pia waliingia
katika orodha ya wafungaji katika mchezo huo wa ufunguzi wa Kundi G.
Huo n mwanzo mzuri katika mchezo wa kwanza wa
kimashindano kwa kocha Julen Lopetegui, ambaye alihusika kwa timu yake kupata
ushindi kiduchu baada ya kuwa mbele kwa bao 1-0 hadi kipindi cha kwanza
kinamalizika.
Matokeo hayo yaliwafanya kuwa vinara wa awali
wa Kundi G lakini Italia nayo ilianza kwa ushindi wa 3-1 licha ya kujkuta
ikipunguzwa na kubaki na wachezaji 10 walipocheza dhidi ya Israel katika mchezo
uliofanyika Haifa.
Graziano Pelle alikiwezesha kikosi cha kocha Giampiero
Ventura kuanza vizuri kampeni zake kabla Antonio Candreva hajaongeza bao
jingine alilofunga kwa penalti na kuihakikishia ushindi timu hiyo.
Tal Ben Chaim aliifungia Israel bao la
kufutia machozi lakini Ciro Immobile aliongeza na kuifanya Italia kukamilisha
ushindi wake wa mabao 3-1 licha ya kutolewa kwa mchezaji wake Giorgio
Chiellini.
Mchezo mwingie wa kundi hilo haukumalizika
wakati Albania ikicheza na wajirani zao wa Macedonia huko Shkoder ilibidi
kusimamishwa baada ya dakika 77 kufuatia mvua kubwa kunyesha.
Wakati mchezo huo unasimama timu hizo
zilikuwa zimefungana bao 1-1 kwa bao la Ergjan Alioski ambalo lilikuwa linajibu
lile la Armando Sadiku alilofunga mapema.
Kosovo nao ilianza vizuri kucheza mashindano
hayo ya kufuzu kwa Kombe la Dunia baada ya kutoka nyuma na kulazimisha sare ya
kufungana bao 1-1 katika mchezo wao wa kwanza wa kufuzu katika mchezo
uliofanyika Finland.l
Mchezaji wazamani wa Norway Valon Berisha – mmoja kati ya wachezaji
sita walihalalishwa kucheza saa chache kabla ya kuanza kwa mchezo huo, alifunga
bao la kusawazisha kwa penalti baada ya dakika 60.
Paulus Arajuuri aliipatia Finland bao la
kuongoza katika mchezo wa Kundi I, lakini Kosovo, ikicheza mchezo wake wa
kwanza wa mashindano ya kimataifa, ilicheza vizuri na walipiga mwamba kupitia
kwa Leart Paqarada kabla Berisha hajaiwezesha timu hiyo kuondoka na pointi.
Hiyo ni moja kati ya sare tatu za 1-1 katika
kundi hilo, huku zingie zikiwa ni kati ya Croatia na Uturuki huko Zagreb na Ukraine
na Iceland huko Kiev ambazo nazo zilimalizika kwa sare kama hiyo.
Katika Kundi D, mbaop kutoka kwa Martin
Hinteregger na Marc Janko yaliisaidia Austria kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi
ya Georgia huko Tbilisi.Bao la kufutia machozi lilifungwa na Jano Ananidze.
Kwingineko katika Kundi D, Ireland ilitoka
sare ya kufungana mabao 2-2 na Serbia huku Wales ikiichapa Moldova 4-0.
No comments:
Post a Comment