Saturday, 17 September 2016

Kongamano la Michezo lajadili kwa kina kuporomoka kwa michezo hapa nchini na kuibuka na jibu zito



Vyeti vya wakongwe wa michezo hapa nchini, Chabanga Hassan Dyamwale na Khalfa Abdallah.

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imesema kuwa kunatakiwa uwekezaji mkubwa kuendeleza michezo hapa nchini  ili kuzalisha ajira na kuongeza pato la taifa, imeelezwa.

Hayo yamo katika hotuba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye iliyosomwa na Mkuruenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Petro Lyatuu.

Washiriki wa Kongamano la michezo nchini wakiwa katika picha ya pamoja baada ya konamalo hilo kufunuliwa katika shule za Filbert Bayi Mkuza, Kibaha mkoani Pwani.
Nape alisema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kuendeleza michezo hapa nchini na mpango wa maendeleo wa taifa wa miaka mitano (2016-2017-2020-2021) unatambua Tanzania bado iko nyuma katika michezo na hivyo kunahitajika uwekezaji wa makusudi ili kuinua kiwango cha michezo hapa nchini.

Alisema kuwa mafanikio ya michezo hapa nchini katika miaka ya nyuma hayakuja kimiujiza, kwani kulikuwa na programu maalumu zilizowezesha vijana kushiriki katika michezo kama mashindano ya Shule za Msingi na Sekondari ya   Umitashumta na Umisseta.

Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), Amir Mhando akichania mada wakati wa Konamano la Michezo lililofanyika katika shule za Filbert Bayi Mkuza, Kibaha mkoani Pwani. Kushoto ni mwanariadha wazamani, Gidamis Shahanga.
Alisema kuwa vionozi wazamani wa michezo hawakuwa na tamaa wakati wa uongozi wao hawakuwa na tamaa ya fedha au madaraka waliyopewa ya kusimamia michezo kama ilivyojitokeza sasa katika klabu na taasisi zinazojaribu kufufua michezo hapa nchini.



Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Gulam Rashid alisema kuwa michezo hapa nchini ilishuka kuanzia katika miaka ya 1990 ukilinganisha na miaka ya 1970-80 huenda ilitokana na mifumo ya Serikali kuwa tofauti katika kuchangia michezo kwa ujumla.

Gulam alisema kuwa wakati huo kulikuwa na taasisi mbalimbali kama Mamlaka ya Bandari, Kampuni za Mafuta kama Esso, Majeshi (JWTZ), Polisi, JKT, Magereza, Uhamiaji zilikuwa na timu za michezo mbalimbali, ambzo zilileta ushindani na kusababisha kuendelea kwa michezo hapa nchini.

Alisema wanamichezo huandaliwa kuanzia chini, ambapo hakuna ubishi kuwa nazi hizi ni shuleni, ambako kulikuwa na vipindi vya elimu ya viungo kwa wanafunzi wetu.

Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Muchezo la Taifa (BMT), Mohamed Kiganja akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Akichangia mada katika kongamano hilo, kaimu katibu mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa, BMT, Mohamed Kiganja alisema upatikanaji wa viongozi wa michezo hapa nchini ni mbovu sana kiasi cha kuingiza watu wasio na uzalendo au kuongoza licha ya kuwa na elimu ya kutosha.

Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), Amir Mhando alisema viongozi wengi wa vyama vya michezo hawana hasa nia ya kuendeleza michezo ila wengi wao lengo lao ni kutaka kutoka kimaisha kupitia michezo.
Alisema wengi wamekuwa wakiingia kuongoza michezo ili kujitafutia njia ya kuingia katika siasa katika ngazi tofauti tofauti.
Mkurugenzi wa kwanza wa michezo nchini, Khalfa Abdallah akitoa neno la shukrani wakati wa ufunguzi wa kongamano la michezo nchini lililofanyika katika shule za Filbert Bayi Kibaha.
Mkurugenzi wa kwanza wa michezo mzalendo, Khalfa Abdallah alitaka kongamano hilo liwe chachu kwa makongamano mengine ambayo yanatakiwa kuandaliwa na Serikali ili kupata jibu la kufanya vibaya katika michezo.

Abdallah aliongoza ofisi hiyo kuanzia mwaka 1964 hadi mwaka 1990 alipostaafu.

Baadhi ya wadau wengine wa michezo walioshiriki kongamano hilo ni pamoja na Leonard Thadeo aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Michezo nchini, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Makoye Nkenyenge, mkurugenzi wa Chuo cha Michezo cha TOC Suleiman Jabir, mkimbiaji wazamani Gidamis Shahanga na Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Petro Lyatuu akifungua kongamano la michezo Mkuza, Kibaha jana.
 Kongamano hilo linatarajia kumalizika leo, ambapo suluhisho la nini kifanyike ili kuendeleza michezo hapa nchini baada ya michezo kuporomoka kwa miaka mingi.
 Mkurugenzi wa kwanza wa michezo nchini, Khalfa Abdallah (kushoto) na meneja wa kwanza wa Uwanja wa Taifa (sasa Uhuru), Chabanga Hassan Dyamwale wakiteta wakati wa mapumziko ya Kongamano la Michezo katika Shule za Filbert Bayi Kibaha jana.
 Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi akizungumza wakati wa kongamano hilo.
Mwenyekiti wazamani wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), Anna Bayi akizungumza na mwanamichezo wazamani, Chabanga Hassan Dyamwale. Kushoto ni Mkurugenzi wa kwanza wa Michezo, Khalfa Abdallah.


No comments:

Post a Comment