Washiriki wa Bonanza la uzinduzi wa mashindano ya Shimiwi wakipita katika barabara ya Mandera leo kuelekea Uwanja wa Uhuru. |
Na Mwandishi Wetu
KATIBU Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi leo alikuwa
mgeni rasmi katika Bonanza la uzinduzi wa mashindano ya 34 ya Shirikisho na Taasisi
za Umma (Shimiwi), lililofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Utumishi, Lauriane Ndombaro akimkabidhi Kombe la ushindi wa kwanza Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva. |
Kijazi ambaye hotuba yake ilisomwa na Katibu Mkuu wa
Utumishi, Dkt Laurean Ndumbaro, ambayo iliwataka waajiri kuwatimizia mahitaji
wafanyakazi wao ili waweze kujiandaa na kushiriki vizuri katika mashindano ya
Shimiwi, ambayo mwaka huu yatafanyika Dodoma baadae mwezi ujao.
Alisema kuwa
waajiri wanatakiwa kuwa patia mahitaji muhimu kama vifaa vya michezo na
mahitaji mengine ili wafanyakazi wao waweze kushiriki vizuri katika mashindano
hayo, ambayo mwaka jana hayakufanyika ili kupisha Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabune
na Madiwani hapa nchini.
Dokta Mtaka akimchua mmoja wa washiriki katika bonanza hilo la ufunuzi wa Shimiwi leo Jumamosi. |
Kijazi pia alimpongeza Rais wa awamu ya tano wa
Tanzania Dkt Pombe Maufuli kwa jitihada zake za kuliletea maendeleo ya haraka
taifa la Tanzania, ambapo hadi sasa amefanya mambo mengi.
Pia aliwataka wafanyakazi hao wa umma kuwa na nidhamu
wakati wote wa mashindano hayo ili kuonesha taswira nzuri kwa jamii.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakifanya mazoezi katika bonanza hilo leo. |
Pia aliwataka wafanyakazi hao wa umma kufanaya
mazoezi kila wakati sio kusubiri tu wakati wa bonanza hilo au mashindano ya
Shimiwi kwani mazoezi uwajena kimiili na kiakili na kuwawezesha kufanya kazi
kwa ufanisi zaidi.
Aliwaambia kuwa michezo inawaepusha wafanyakazi hao
wa Serikali na maonjwa yasiyoambukiza kama shinikizo la damu, kisukari, kupooza
na mengine mengi.
Katika bonanza hilo viongozi mbalimbali wa wizara na
taasisi mbalimbali za Serikali walishirriki katika bonanza hilo ambalo lilianza
kwa washiriki zaidi ya 2,000 kukimbia katika mitaa mbalimbali ya jirani na
Uwanja wa Uhuru na kurudi katika uwanja huo ambako walifanya mazoezi ya viungo
kabla ya mgeni rasimu kuzungumza.
Mbali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Elisante Ole Gabriel, viongozi wengine waliokuwemo uwanjani hapo leo ni pamoja na katibu mkuu wa uchukuzi Dkt. Leornard Chamuriho (kulia) na katibu
mkuu wa Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora.
Aidha, Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es
Salaam (RAS) ndio ilitwaa ushindi wa kwanza katika shindano la taasisi
iliyoshirikisha wafanyakazi wake wengi katika bonanza hilo la uzinduzi wa
mashindano ya 34 ya Shimiwi baada ya kuwa na wafanyakazi 180 huku Kilimo
walimaliza wa pili kwa kuwa na wafanyakazi 82.
Mwakilishi wa Kilimo (kulia) akipokea Kombe la ushindi wa pili kutoka kwa Katibu Mkuu Utumishi. |
Washindi hao wa kwanza na pili walipewa zawadi ya
makombe, ambayo yatakuwa yao kabisa.
Naye mwenyekiti wa Shimiwi Daniel Mwalusambi
aliwashukuru viongozi wote waliowaruhusu wafanyakzi wao kushiriki bonanza hilo
la uzinduzi wa mashindano ya Shimiwi.
Pia aliwataka kuwawezesha na kuwaruhusu kushiriki
mashindano ya Shimiwi mkoani Dodoma mwaka huu.
Mwenyekiti wa Shimiwi, Daniel Mwalusambi akizungumza leo kwenye Uwanja wa Uhuru |
MC wa Bonanza hilo la uzinduzi, ambalo lilifana, Joyce Benjamin. |
No comments:
Post a Comment