NAHODHA wa Manchester United Wayne Rooney jana nusura azichape na
kocha wa Man City Pep Guadiola wakati timu hizo zikipambana katika mchezo wa
Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Huku Man United ikiwa nyuma kwa bao 1-0 mchezo huo ukielekea
katika katika ya kipindi cha pili, Rooney alijaribu kuchukua mpira uliotoka
baada ya kuchuana na mchezaji mmoja wa Man City.
Guardiola, akiwa katika eneo lake la ufundi, aliokota mpira huo na
kuonekana kama alitaka kumpa mchezaji huyo.
Lakini Kocha huyo wa Man City alikataa kukabidhi mpira huo kwa Rooney
na badala yake aliuweka nyuma ya mchezaji huyo ili asiuchukue haraka.
Rooney alijaribu kuuchukua mpira kwa nguvu, akionekana kupokonya
mpira huo na kumsukuma Guardiola, kabla kocha huyo Mhispania kuwa mpole na
kuuachia mpira huo.
Mwamuzi wa mchezo huo Mark Clattenburg, alikuwa mstaarabu pamoja
na kushuhudia tukio hilo, kabla hajawashika mkono mmoja baada ya mwingine.
Man City ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Man United katika mpambano
wa kwanza wa Manchester msimu huu, shukrani kwa mabao ya kipindi cha kwanza
kutoka kwa Kevin De Bruyne na Kelechi Iheanacho.
Zlatan Ibrahimovic aliipatia Man United bao la kufutia machozi muda
Mfupi kabla ya mapumziko huku kikiwa hakia bao lolote.
Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Man United chini ya kocha wao mpya
Mreno Jose Mourinho.
No comments:
Post a Comment