Wananchi wa Vunezuela wakiwa katika mstari mrefu kwa ajili ya kunua bidhaa mbalimbali ikiwemo sukari iliyoadimika. |
CARACAS, Venezuela
UPUNGUFU wa sukari umelazimisha Coca-Cola kusimamisha
uzalishaji wa vinywaji nchini hapa kutokana na matatizo ya chakula na nishati.
Coke katika taarifa yake ilisema kuwa
Venezuela kwa muda itasimamisha uzalishaji kutokana na upungufu wa mali ghafi.
Tangazo hilo limekuja baada ya kampuni hiyo
kubwa ya vinywaji, Empresas Polar, kufunga kiwanda kutokana na upungufu huo
mkubwa wa sukari.
Uchumi wa Venezuela umeporomoka kwa haraka
kutokana na bei ya mafuta kuyumba.
Msemaji wa Coca-Cola alisema kuwa kampuni
hiyo itaendelea kuzalisha vinywaji visivyo na sukari kama Coca-Cola Light (Diet
Coke).
Uzalishaji wa miwa umeporomoka kutokana na kudhibitiwa
kwa bei na kupanda kwa gharama za uzalishaji, pamoja na upatikanaji wa mbolea.
Matokeo yake, wakulima wengi wadogo wamehamia
katika uzalishaji wa mazao mengine ambayo bei yake haidhibitiwi, ambayo pia
huwapatia kipato kikubwa.
Venezuela ilitarajiwa kuzaliwa tani 430,000 za
miwa mwaka 2016/17, badala ya tano 450,000 kwa miezi 12 iliyopita, na kuingiza tani
850,000 ya malighafi na sukari iliyokuwa tayari imeshatengenezwa kwa mujibu wa
takwimu za USDA.
Matatizo ya kiuchumi yamesababisha wananchi
wengi kujipanga katika misururu mirefu kwa saa kadhaa wakinunua mahitaji ya
nyumbani.
No comments:
Post a Comment