Na Mwabndishi Wetu
MUIMBAJI nguli wa mashairi nchini, Mrisho Mpoto amesema kuwa
atatumia kipaji chake cha uimbaji kutunga nyimbo za kupambana na unyanyapaa kwa
watu wenye virusi vya Ukimwi.
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Watu wenye ulemavu, Dk. Abdallah Possi akifungua mkutano wa mwaka wa masuala ya Vijana leo jijini Dar es Salaam. |
Mpoto ambaye anajulikana sana kama Mjomba aliyasema hayo jana
wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Masuala ya Vijana uliofanyika Ubingo Plaza jijini
Dar es Salaam.
Mjomba alisema alizitaka taasisi na watu mbalimbali kuchangisha
fedha kwa ajili ya kuzisaidia taasisi mbalimbali zinazoshiriki kusaidia
waathirika wa Ukimwi.
Msanii huyo ambaye ni Balozi wa Kili Challenge,ambayo inahusika na
kuchangisha fedha kupitia upandaji Mlima Kilimanjaro.
Alisema kuwa wafadhili kutoka nje ambao wanasaidia kuchangia mfuko
huo wa kusaidia waathirika, siku moja wataacha kusaidia, hivyo aliwataka
Watanzania kuchangia mfuko huo.
Alisema kuwa unyanyapaa ndio kimekuwa kitu hatari zaidi kwa jamii,
hivyo aliwataka watu kuacha tabia ya kuwatenga wenye maambikizo na kushirikiana
nao katika shughuli mbalimbali.
Mjomba hivi karibuni aliteuliwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM)
na Tume ya Kupambana na Ukimwi Tanzania (Tacaids) kuwa balozi wa Kili
Challenge.
Akizungumza baada ya ufunguzi huo, msanii wa BongoFleva Banana
Zorro alisema kuwa atajitahidi kuwaelimisha wapenzi wa muziki kuhusu madhara ya
unyanyapaa.
Naye naibu waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Walemavu, Abadllah Posi alisema vijana wanatakiwa kujiepusha na madawa ya
kulevya na pombi kwani ndivyo vyanzo vikubwa vya Ukimwi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Fatma Mrisho alisema vijana hasa
wanawake ndio waathirika wakubwa wa ugonjwa huo hapa nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Fatma Mrisho akizungumza katika mkutano wa mwaka wa wadau wa vijana leo. |
No comments:
Post a Comment