LONDON, England
KOCHA wa Manchester
United Louis van Gaal anasema mashabiki wa timu hiyo walitarajia mambo makubwa kutoka katika klabu
hiyo ya Old Trafford.
Man United iliifunga
Bournemouth jana na kumaliza ya tano katika Ligi Kuu ya England, lakini
mabingwa hao mara tatu wa Ulaya wamekosa nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa wa
Ulaya kwa mara ya pili katika misimu miwili.
"Timu yetu
iko katika mpito na na kama nilivyosema tangu mwanzo, “alisema
Van Gaal, ambaye alianza kuifundisha timu hiyo katika kipindi cha majira ya
joto ya mwaka 2014.
"Labda
nilihitajika kutuma ujumbe mzuri zaidi ya nilivyofanya.”
Kocha wazamani wa
Uholanzi Van Gaal alisaini mkataba wa miaka mitatu baada ya kuichukua timu hiyo
miezi mitatu tangu alipotimuliwa David Moyes, ambaye aliitumikia timu hiyo
miezi 10 akichukua nafasi ya kocha Sir Alex Ferguson.
Haijulikani kama
Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 64 kama atashuhudia msimu wake wa mwishio Old
Trafford, ingawa alisema kuwa anaamini ataendelea kuifundisha timu hiyo hadi
atakapomaliza mkataba wake.
Baadhi ya
mashabiki wa Man United wamemtaka kuondoka kocha huyo wazamani wa Ajax,
Barcelona na Bayern Munich kuondoka, wakati baadhi yao wakizomea katika mchezo
wa mwisho wakishinikiza aondoke katika mchezo dhidi Bournemouth.
Van Gaal anaweza
kuiongoza Man United kutwaa taji lake kubwa la kwanza tangu mwaka 2013 – taji
la Ligi Kuu ya England chini ya Ferguson – wakati
Jumamosi
watakapokabiliana na Crystal Palace katika fainali ya Kombe la FA
kwenye Uwanja wa Wembley.
Lakini alikiri
timu hiyo kumaliza katika nafasi ya tano ni sawa na hatua moja nyuma baada ya kuwaongoza Mashetani hao wekundu
kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa katika msimu wake wa kwanza.
"Lengo letu
katika mwaka wa kwanza na wa pili na watatu ni Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, “alisema
baada ya kushinda 3-1 dhidi ya Bournemouth.
"Ni kiwango
cha juu na klabu kama Manchester United inatakiwa kucheza katika kiwango kama
kile, lakini kuna klabu zaidi ambayo zinazotaka kucheza katika kiwango kile na
hilo umeliona.
"Matarajio ni
makubwa sana. Mashabiki wanatarajia mengi lakini nafikiri matarajio haya ni
makubwa sana.”
No comments:
Post a Comment