KWA Kipindi kirefu sasa Tanzania imeendelea kuwa na watu wengi wanaoishi na Virusi
vya UKIMWI pamoja na wagonjwa wa UKIMWI.Kwa mujibu wa takwimu kutoka Tume ya
Kupambana na UKIMWI nchini (TACAIDS) inakadiriwa kuwa watu milioni 1.6 nchini
wanaishi na VVU na Ukimwi. Ugonjwa huu umewaathiri zaidi vijana na watoto
yatima zaidi ya milioni 1.3.
Bado
ipo changamoto miongoni mwa jamii kuhusu elimu ya ugonjwa huo kwa kuwa kuna
vituo vichache sana vya taarifa juu ya janga hilo.Jamii bado ina unyanyapaa kwa
Watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI pamoja na UKIMWI.
Hali hii ndiyo
inayosababisha tuchelewe kukabiliana na janga hili.Waathirika wa tatizo hili
wamekuwa woga kwa hofu ya unyanyapaa miongoni mwa jamii.Usiri huu na elimu
ndogo ya kukabiliana na ugonjwa huu ikiwemo matumizi sahihi ya kinga na dawa za
kupunguza makali yake vimezidi kufanya hali izidi kuwa mbaya
Katika
kukabiliana na changamoto hiyo na kuisaidia serikali kufikia lengo namba tatu
la Malengo endelevu ya Maendeleo ya Umoja wa mataifa ya kuwa na jamii yenye afya bora ifikapo
2030,Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) kwa kushirikiana na Tume ya Kupambana na
UKIMWI nchini (TACAIDS) umendelea tena kuchangisha fedha ili kupambana na
UKIMWI kupitia Kampeni yake ya KILI CHALLENGE.
KILI
CHALLENGE ni kampeni iliyoanza mwaka 2002 ambayo hufanywa kila mwaka kwa wadau
mbalimbali kupanda mlima Kilimanjaro na kuchangisha fedha kwa ajili ya
kutunisha mfuko wa mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI pamoja na UKIMWI.
Mwaka
2015 pekee Kampeni hii ilifanikiwa kukusanya takribani shilingi za Kitanzania
Bilioni Moja. Fedha hizo zitatolewa kwa wadau mbalimbali wanaojishughulisha na
mapambano ya Ukimwi katika uzinduzi wa upandaji Mlima kwa mwaka huu pale Hyatt
Hotel, Dar es Salaam Ijumaa tarehe 20 Mei.
Mgeni rasmi katika Hafla hiyo
atakuwa makamu wa Raisi Mhe. Samia Suluhu.
Makamu
wa Rais wa miradi endelevu wa Anglogold Ashanti (GGM) Bw. Simon Shayo amesema
kuwa Kampeni ya Kili Challenge mwaka huu itakuwa na utofauti mkubwa kwa kuwa
inafanyika chini ya Serikali mpya.
“Kwa miaka 15 iliyopita
tumeshirikiana vizuri na Serikali zote pamoja na wadhamini mbalimbali ambao
wamekuwa wakituunga mkono kutuchangia fedha ili kupambana na tatizo
hili.
Tunaamini kuwa Serikali mpya chini ya Rais
Dkt John Pombe Magufuli ambayo imekuwa ikifanya jitihada nyingi kununua
dawa na kuboresha huduma za Afya itatuunga mkono katika Kampeni yetu mwaka huu.”Anaeleza Bwana Shayo.
Zaidi
ya Asasi 30 zimeweza kunufaika na Mfuko huu katika kipindi cha miaka 15
iliyopita. Baadhi ya asasi hizi ni pamoja na TACAIDS,
Benjamin Mkapa Foundation, Geita Hospital na nyinginezo.
Shayo amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kwa wingi kuchangia fedha katika
Kampeni hiyo ili kusaidia kupunguza ongezeko la maelfu ya watoto yatima
wanaohitaji misaada baada ya wazazi wao kufariki.
Mkurugenzi
Mtendaji wa TACAIDS Dk. Fatma Mrisho amesema, “Tukifanikiwa kushiriki kikamilifu katika
Kampeni hii tutafanikiwa pia kusaidia wajane wasiokuwa na kipato pamoja na
wazee wanaolazimika kuwalea wajukuu walioachwa na watoto ambao walifariki
kutokana kwa ugonjwa huo”
Kilimanjaro
Challenge imebakia kuwa Asasi pekee inayoleta kwa pamoja serikali na Makampuni
binafsi kwa ajili ya mapambano dhidi ya VVU & Ukimwi kwa jamii ya
Kitanzania na dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii
inabaki bila kuathiriwa na ugonjwa huo katika miaka ijayo.
Mpango
huo pia unalenga kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU & Ukimwi sambamba na
kutoa nafasi kwa watalii wa ndani kuupanda mlima Kilimanjaro.
KUHUSU Kili Challenge:
Kwa
maelezo zaidi tembelea tovuti ya www.anglogoldashanti.com na www.geitakilichallenge.com
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:-
Tenga B Tenga – Manager, Public Relations
& Communications
Email: ttenga@anglogoldashanti.com
Tel: +255 282 160 135 | +255
689 103 619
No comments:
Post a Comment