MANCHESTER, England
KOCHA Jose Mourinho (pichani) anakutana na uongozi wa Manchester United leo
kwa ajili ya mazungumzo kuwa mbadala wa Louis van Gaal kama kocha wa timu hiyo.
Van Gaal, 64, alitimuliwa Jumatatu, ikiwa ni siku mbili baada ya
kuiwezesha timu hiyo kutwaa taji la FA, kwa sababu ya kiwango kibovu cha tiu
yake.
Man United ilimaliza ya tano katika msimamo wa Ligi kuu ya England
msimu huu na ilitolewa katika hatua ya makundi ya mashindano ya Ligi ya
Mabingwa wa Ulaya.
Mourinho, 53, mmoja wa makocha aliyepata mafanikio makubwa katika
soka, amekuwa hana kazi tangu Desemba baada ya kutimuliwa Chelsea.
Alishinda mataji matatu ya Ligi Kuu katika vipindi vyake viwili
alivyotua Stamford Bridge, na aliiongoza Porto na Inter Milan kutwaa mataji ya
Ligi ya Mabingwa wa Ulaya mwaka 2004 na 2010.
Kocha hiyo Mreno pia aliiongoza Real Madrid kutwaa taji la
Hispania mwaka 2012, na uteuzi wake utashuhudia muendelea wa upinzani na kocha
wazamani wa Barcelona Pep Guardiola,ambaye ataanza kuifundisha Manchester City
katika kipindi hiki cha majira ya joto.
Kipa wazamani wa Man United Peter Schmeichel amempigia debe Mourinho,
lakini alisema klabu itakubali uteuzi wake.
Mourinho alitimuliwa Chelsea baada ya kuanza vibaya utetezi wao wa
taji la Ligi Kuu, ambapo walishindwa mechi tisa za kwanza kati ya 16.
Pia kocha huyo alijiingiza katika mgogoro mkubwa na daktari wa
timu hiyo Eva Carneiro, ambaye alitimuliwa na alifungua kesi dhidi ya klabu
hiyo akidai kunyanyaswa.
"Mourinho aligombana na mkurugenzi wa soka katika klabu hiyo,
rais, daktari wa timu. Alifanya mambo tofauti na jinsi Manchester United wanataka
klabu yao ya soka iendeshwe,”alisema Schmeichel,
52.
No comments:
Post a Comment