Na Mwandishi Wetu
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan Ijumaa atakuwa mgeni
rasmi katika uzinduzi wa kuchangisha fedha kwa ajili ya kupambana na Ukimwi
utakaofanyika jijini Dar es Salaam, imeelezwa.
Hafla hiyo imeandaliwa na Mgodi wa
Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya Kupambana na Ukimwi
Tanzania (Tacaids),ambapo mwaka huu wanatarajia kukusanya zaidi ya sh. bilioni
1.
Makamu wa Rais wa GGM, Simon Msuya akzungumza na waandishi wa habari mapema leo. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Dk. Fatma Mrisho na Balozi wa Kili Challenge Mrisho Mpoto. |
Mkurugenzi Mtendaji wa Tacaids, Fatma Mrisho alisema jana kuwa GGM
kwa kushirikiana na Tacaids kila mwaka imekuwa ikichangisha fedha kwa ajili ya
kusaidia vituo na taasisi mbalimbali zinazopambana na Ukimwi.
Fedha hizo zitachangishwa kwa utaratibu wa kupanda Mlima
Kilimanjaro, ambapo watu mbalimbali wanatarajia kuchangia, ambapo fedha hizo
zitasaidia vituo mbalimbali vinavyosaidia waathirika wa Ukimwi.
Alisema vifo vitokanavyo na Ukimwi vimepungua kwa takribani
asilimia 40 lakini vinatakiwa kufikia asimilia 100.
Aidha, makamu wa rais wa GGM Simon Shayo alisema kuwa kesho katika
hafla hiyo pia wataitumia kuzipa fedha taasisi mbalimbali za umma na zila za
binafsi zinazopambana na Ukimwi.
Alisema mwaka jana walikusanya kiasi cha Sh Bilioni 1 na mwaka huu
wanatarajia kukusanya fedha zaidi kwa ajili ya kusaidia vikundi au taasisi
zinazopambana na Ukimwi.
Alisema GGM itaendelea kushirikiana na serikali katika vita hiyo
ya kupambana na ukimwi ili kuhakikisha unapungua na kumalizika kabisa ifikapo
mwaka 2030.
Alisema kuwa katika hafla hiyo kesho watatoa fedha zilizokusanywa
mwaka jana kwa taasisi mbalimbali.
Balozi wa Kili Challenge Mrisho Mpoto alisema kuwa jana kuwa jamii bado ina unyanyapaa kwa watu wanaoishi
na Virusi vya UKIMWI pamoja na UKIMWI, ambapo hali hiyo inasababisha kuchelewa
kukabiliana na janga hilo.
Imeelezwa kuwa tatizo hilo limesababisha waathirika wa tatizo hilo
kuwa na woga kwa kuhofia unyanyapaa miongoni mwa jamii, kitu ambacho kinaumiza
sana.
Alisema kuwa, usiri huo na elimu ndogo ya kukabiliana na ugonjwa huo
ikiwemo matumizi sahihi ya kinga na dawa za kupunguza makali yake vimezidi
kufanya hali izidi kuwa mbaya.
Alisema atajitahidi kuhakikisha uteuzi wake unakuwa na matokeo
chanya katika jamii, hasa vijana ambao ndio waathirika wakubwa wa ugonjwa huo
hapa nchini.
Kwa kipindi kirefu sasa Tanzania imeendelea kuwa na watu wengi
wanaoishi na Virusi vya Ukimwi pamoja na wagonjwa wa Ukimwi.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Tacaids, inakadiriwa kuwa watu
milioni 1.6 nchini wanaishi na VVU na Ukimwi, na kuwaathiri zaidi ya vijana na
watoto yatima milioni 1.3.
Bado ipo changamoto miongoni mwa jamii kuhusu elimu ya ugonjwa huo
kwa kuwa kuna vituo vichache sana vya taarifa juu ya janga hilo.
No comments:
Post a Comment