Baadhi ya wanariadha wakichuana katika mbio za Ngorongoro Marathoni 2012 na mbio hizo zimeendelea kukuwa kila mwaka na kushirikisha washiriki kibao kutoka ndani na nje ya nchi. |
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Jumanne Maghembe amethibitisha kuanzisha msimu wa tisa wa mbio za Ngorongoro Marathon zitakazofanyika Aprili 16.
Mmoja wa waratibu wa mbio hizo, John Mbando alisema kuwa,
Maghembe amethibitisha kuwa mgeni rasmi wa mbio hizo za kila mwaka.
Mwanariadha wa kimataifa wa Tanzania, Fabian Joseph akimaliza mbio za Ngorongoro Marathon 2012 kwenye Uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu |
Mbio za mwaka huu zinatarajia kuwa na msisimko mkubwa na zitashirikisha
zaidi ya wanariadha 2,000 kutoka nje na ndani ya Tanzania.
Mbando alisema kuwa mbio hizo zitaanzia katika lango kuu la
kuingilia na kutokea katika Hifadhi ya Ngorongoro na kumalizia kwenye viwanja
vya Mazingira Bora mjini Karatu mkoani Arusha.
Kampuni mbalimbali zimekuwa zikijitokeza kudhamini mbio hizo. Pichani Tigo walipodhamini mbio za mwaka 2013. |
Mbali na kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa kimaasai,
pia mbio hizo zinasaidia kupiga vita ugonjwa hatari wa malaria kwa kuwaelimisha
watu na kutoa vyandarua.
Mshindi wa kwanza katika mbio za kilometa 21 kwa upande wa
wanawake na wanaume, kila mmoja ataondoka na sh. 2,000,000 huku mshindi wa pili
ataondoka na sh. 1,000,000 na watatu sh. 500,000.
Zaidi ya sh. Milioni 6 zimetengwa kwa ajili ya zawadi za washindi,
ambapo pia kutakuwa na mbio za kilomita tano na zile za wanafunzi wa shule za
msingi na sekondari za kilomita 2.5.
Mbio za mwaka huu zinadhaminiwa na Maji ya Kilimanjaro pamoja na Zara Tours na Zara Charity za zingine.
Mbio za mwaka huu zinadhaminiwa na Maji ya Kilimanjaro pamoja na Zara Tours na Zara Charity za zingine.
Kabla ya kuanza kwa mbio za Ngorongoro 2013 katika lango kuu la kuingilia na kutokea katika Hifadhi ya Ngorongoro |
Nyalandu akimkabidhi zawadi mshindi wa mbio za Ngorongoro 2013 Dickson Marwa. Kushoto ni Alphonce Felix mshindi wa pili wa mbio hizo. |
Wanariadha wakichuana katika mbio za Ngorongoro 2013. |
No comments:
Post a Comment