Na Faki Mjaka-Maelezo
Zanzibar
IDARA ya Mipango Miji
na Vijiji Zanzibar kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Zanzibar
wanatarajia kuanzisha Kituo cha Mtandao wa Taarifa za Maeneo na Mazingira ya
Zanzibar ambapo Wananchi watalazimika kupata taarifa kupitia kituo hicho.
Taarifa hizo zitawekwa
katika mfumo wa kidigitali na kuwekwa katika Mtandao huo ili kuepusha
upotoshaji wa taarifa na pia zipatikane kwa wakati bila ya usumbufu.
Mkurugenzi wa Mipango
miji na Vijiji Zanzibar Dkt. Mohammed Juma ameyasema hayo wakati wa warsha ya
kuandaa utaratibu wa kuanzisha kituo hicho cha Mtandao Shangani mjini Zanzibar.
Amefahamisha kuwa
kutokana na kuwepo kwa Vyanzo vingi vya Taarifa zinazohusu Maeneo ya Zanzibar
kunapelekea baadhi ya Taarifa hizo kutokuwa sahihi na kupelekea mkanyiko katika
jamii.
“Kwa sasa kuna Vyanzo
vingi vya kujua maeneo na mazingira ya Zanzibar..kwa mfano ukienda kutaka
taarifa juu ya eneo fulani inawezekana taarifa hiyo ikatofautiana na Vyanzo
vingine lakini tutakapokuwa na Chanzo kimoja taarifa zitakuwa moja na
sahihi”Alisema Dkt Mohamed.
Ametaja faida
zitakazopatikana kupitia Mtandao huo kuwa nipamoja na kuwarahisishia Wananchi
kupata taarifa popote walipo na kwa wakati kinyume na ilivyo sasa ambapo
hulazimka kwenda katika Taaisi husika jambo ambalo huwaletea usumbufu.
Aidha amesema pia
itakuwa ni sehemu ya uwazi kwa Serikali kupitia Taasisi zake ambapo kila kitu
kitawekwa wazi na kupatikana kirahisi kupitia Mtandao huo.
“Mtandao huo utaweka
wazi maeneo yote yakiwemo,Makaazi,maeneo ya uwekezaji..isipokuwa yale
yakiusalama ili kumrahisishia mwananchi kuweza kupata Taarifa bila kuhangaishwa
huku na kule” alibainisha Dkt Mohammed.
Aidha amebainisha kuwa
katika Warsha ya kuandaa Mtandao huo Taasisi nane zimeshiriki ili kuwa na sauti
moja juu ya maeneo na mazingira ya Zanzibar.
Amezitaja taasisi hizo
kuwa ni pamoja na Mamlaka ya usimamizi wa ardhi, Idara ya Mazingira, Idara ya
Misitu na maliasili zisizorejesheka na idara ya maendeleo ya uvuvi.
Taasisi zingine ni
pamoja na Idara ya Rasilimali za baharini, Chuo kikuu cha taifa SUZA na Mamlaka
ya Mazingira Zanzibar (ZEMA) ambazo zote zimeshiriki katika Mpango huo wa
kuandaa Taarifa za pamoja.
Jumla ya shilingi
Milion 140 zitatumika kuanzisha Kituo hicho cha Mtandao ambazo ni msaada kutoka
Serikali ya Finland.
Kwa upande wake
Mwezeshaji wa mafunzo kutoka Taasisi ya Mazingira ya Finland Bi Riihz
Teinirants amesema Taasisi watendaji wa Taasisi hizo walioshiriki mafunzo
wanajukumu la kuwafahamisha wenzao ili kutimiza lengo lililokusudiwa.
Aidha bi Riihz amesema
mbali na kutoa mafunzo ya kuanzisha Kituo hicho cha Mtandao wataisaidia
Zanzibar kutafuta taarifa za maeneo yake na kuziweka katika Kituo hicho hasa
zile za mwambao wa bahari ili kuleta ufanisi unaohitajika.
Kunzishwa kwa kituo
hicho cha Mtandao wa Taarifa za maeneo ya Zanzibar ni matokeo ya kukamilika kwa
Mradi wa kutunza mazingira Zanzibar (SMOLE) uliofadhiliwa na Serikali ya
Finland katika kuisaidia Zanzibar ambapo Mradi huo ulipata mafanikio makubwa.
No comments:
Post a Comment