LONDON, England
MTENDAJI Mkuu wa Chama Soka England (FA), Martin Glenn amekanusha
mpango wa kuanzisha mashindano ya Ulaya ya Super Cup, akisema kuwa yataua
ushindani.
Klabu kubwa za Ligi Kuu wiki hii zilifanya kikao cha kujadili
mpango wa kuwa na mashindano ambayo yatashirikisha timu kubwa za bara la Ulaya.
Lakini Glenn alisema kusimamisha ligi kwa ajili ya kuziwezesha
baadhi ya timu kushiriki mashindano hayo kutawaweka kando mashabiki.
"Soka linatakiwa kuhusishwa (lakini) hatuwezi kupoteza misingi
ya kupanda na kushusha timu, “alisema
Glenn.
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal na yule wa Arsenal tayari
wameweka wazi kupinga Super Leaguehiyo ya Ulaya.
Glenn, aliyechaguliwa mwaka mmoja uliopita, alitolea mfano vinara
wa Ligi Kuu ya Leicester, ambao hawataweza kujiuna na timu hizo kubwa hata kama
watashinda taji.
Aliongeza pia kusema jinsi mapato ya TV yanapogawanywa sawa kwa
klabu kunaziwezesha timu kama Mbweha hao kuwa na kiwango walichonacho sasa.
Kikao hicho cha "siri" cha klabu kubwa tano za England kimezua
madala. Martin Glenn ni `mzito’ wa hivi
karibuni kukosoa mpango huo wa kuanzisha ligi hiyio ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment