Rais wa Marekani, Barack Obama akisalimia na baadhi ya wafanyakazi na familia zao nchini Cuba. |
HAVANA, Cuba
RAIS wa Marekani Barack Obama amewasili nchini Cuba kwa ziara ya
kihistoria katika kisiwa hicho na kuzungumza na kiongozi wa Kikoministi.
Hii ni mara ya kwanza kabisa kwa rais wa Marekani kutembelea Cuba
tangu yalipofanyika Mapinduzi ya mwaka 1959.
Akizungumza wakati wa kufungua tena ofisi ya ubalosi wa Marekani
jijini hapa, aliita ziara hiyo kuwa ni ya “kihistoria”. Pia alitumia muda fulani katika katika jiji hilo kongwe.
Obama alikutana na Rais wa Cuba Raul Castro, lakini hakukutana na
mwanamapinduzi mstaafu Fidel Castro, na wawili hao watazungumzia pia masuala ya
biashara na mabadiliko ya siasa.
Rais huyo wa Marekani alitoka katika ndehe yake ya Air Force One akiwa
na mkewe Michelle na watoto wake wawili wakike Sasha na Malia.
Akiwa ameshikilia mwamvuli, wawili hao walitembea wakielekea
katika zuria jekundu akisalimiwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Bruno
Rodriguez.
"Tukirejea nyuma mwaka 1928, Rais [Calvin] Coolidge alikuja
hapa kwa meli ya kivita. Ilimchukua siku tatu kufika hapa, lakini mimi
imenichukua saa tatu tu, Air Force One kutua Cuba na hii ni kituo chetui cha
kwanza tangu tulipopaa.”
Baadae Obama alianza kutembelea jiji la zamani la Havana.
No comments:
Post a Comment