1.
Kamishna Msaidizi na Msemaji wa Jeshi la
Polisi, Barnabas Mwakalukwa akinyanyua juu moja ya bunda la Dola za Kimarekani
zilizokamatwa leo kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere
(JNIA), zikisafirisha isivyo halali na raia wa Sudan Kusini Bi. Nada Zaelnoon
Ahamed na Bw. Mohamed Belal, raia wa Syria.
Na Mwandishi Wetu
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
mikutano wa Jengo la Pili la abiria la JNIA, Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Kamishna Msaidizi, Barnabas Mwakalukwa alimtaja Raia wa Sudan Kusini Bi. Nada
Zaelnoon Ahamed (38) mwenye hati ya kusafiria namba P01563534 amekamatwa saa
10:00 jioni akiwa eneo la ukaguzi wakati akiingia ndani tayari kusafiri kwa
ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ 485) akielekea Nairobi.
1.
Bi.Nada Zaelnoon Ahamed (38) Raia wa
Sudan Kusini (katikati mwenye ushungi) akiwa mbele ya waandishi wa habari
kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la abiria la Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), baada ya kukamatwa na dola 60,000 za
Kimarekani na Paundi 3410 za Sudan.
Hatahivyo, Afande Mwakalukwa amesema abiria huyo
am3kamatwa na dola 60,000 za Kimarekani na paundi za Sudan 3410, ambazo zote
kwa pamoja alishindwa kutoa taarifa ya fedha alizokutwa nazo kwa mujibu wa
sheria ya utakatishaji fedha ya mwaka 2006 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012.
Pia alimtaja Bw. Mohamed Belal (31), Raia wa Syria
mwenye hati ya kusafiria namba 003-16L096876 aliyekuwa akisafiri kwa ndege ya
Shirika la ndege la Ethiopia (ET 864) kuelekea Syria kupitia Addis Ababa
amekamatwa na dola za kimarekani 10,000 sawa na Tsh. milioni 20 za Kitanzania,
ambazo naye alishindwa kuzitolea taarifa.
“Watuhumiwa wote wawili wamezuiwa na hawawezi
kuendelea na safari zao kwa ajili ya uchunguzi zaidi na hatua za kisheria
zilizopo,” amesema Afande Mwakalukwa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), Bw. Richard Mayongela amewapongeza maafisa usalama wa JNIA kwa
kufanya kazi kwa weledi na uadilifu pamoja na kushirikiana na vyombo vingine
vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha wasafiri, wadau na maeneo yote ya
viwanja vya ndege yanabaki salama na vitendo vya kiuhalifu havina nafasi katika
viwanja hivyo.
1.
Jumla ya Dola za Kimarekani 70,000 sawa
na Tsh. milioni 156 za Kitanzania zikiwa zimekamatwa leo kwenye Kiwanja cha
Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), zikisafirishwa na Raia wawili wa
Syria Bw. Mohamed Belal na Bi. Nada Zaelnoo Ahamed raia wa Sudan Kusini kwa kutofuata
taratibu.
Ametoa wito kwa wadau, wasafiri na wafanyakazi wote
kushirikiana na maafisa usalama, vyombo vya ulinzi na usalama katika kutoa
taarifa stahiki ili vitendo vya kiuhalifu kama hivi visipate nafasi kwenye
viwanja vya ndege kwani ndio vinatoa taswira ya nchi.
“Viwanja vya ndege visitumike kama uchochoro wa
kupitisha nyara za serikali, dawa za kulevyia, fedha haramu au matukio yeyote
yanayoashiria uvunjifu wa Amani au uvunjaji wa sheria za nchi,”
Pia aliongeza “Niombe wananchi na vyombo vya usalama
kufanya kazi kwa weledi kwa sababu wasipofanyakazi kwa weledi matukio kama haya
yangeweza kupata nafasi na kuharibu taswira ya nchi, kwa ujumla mwisho wa siku
inaharibika, kwani nia yetu na lengo letu ni zuri ni kuhakikisha hatutumiki kwa
namna moja au nyingine kufadhili au kuwezesha shughuli za kiuhalifu zifanyike
katika maeneo yetu”.
Amesema na hii ni moja ya ushahidi maafisa usalama
wanapata mafunzo na kujengewa uwezo wa kuwa na vifaa vya kisasa kwani vitu
mbalimbali vimekuwa vikigundulika kupitia mashine za ukaguzi, na pia
kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, hivyo ametoa wito watu
wasidhubutu tena kujaribu kwa namna yeyote ile akidhani viwanja vya ndege
wamelala, kwani ulinzi na usalama unaendelea kuimarika.
Kwa upande wake Meneja wa Forodha wa Kituo cha JNIA,
Bw. Njaule Mdendu amesema abiria wote wanaosafiri au kuwasili endapo wanakiasi
kikubwa cha fedha za kigeni kuanzia dola 10,000 za Kimarekani sawa na Milioni
10 za Kitanzania anapaswa kutoa taarifa Idara ya Forodha kwa kuwa ni matakwa ya
sheria ya mwaka 2006 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2012 na kanuni za mwaka
2016, na asipofanya hivyo ni kosa la jinai.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha (kushoto) akimsikiliza
Kamishna Msaidizi wa Polisi, Barnabas Mwakalukwa (aliyesimama) alipokuwa akitoa
maelezo kwa waandishi wa habari leo ya kukamatwa kwa Raia wawili wa Sudan
Kusini na Syria waliokuwa wakisafirikisha fedha taslim milioni 156 bila kufuata
sharia.
Bw. Mdendu amesema abiria wanapaswa kuchukua fomu
maalum akieleza utambulisho wake na kiasi cha fedha anachoingia nacho au kutoka
nacho, na fomu atazipata kwenye ofisi zote za forodha za mipakani kwenye
viwanja vya ndege, mipaka ya ardhi na majini endapo atakuwa akitumia usafiri wa
barabara au majini.
“Hizi fomu pia zipo kwenye tovuti ya Mamlaka ya
Mapato Tanzania na akishajaza anawasilisha ofisi za Forodha na kiasi cha fedha
anachosafiri au kuwasili nacho na afisa atazihakiki na akiridhika ataruhusu
aendelee na safari yake, na napenda kuwatoa hofu watu kuwa fedha zao
hawanyang’anyi baada ya kutoa taarifa na ataondoka nayo, lakini endapo usipotoa
taarifa ni kosa na inaadhabu yake kulingana na kiasi cha fedha ulichokutwa
nacho, hivyo tuwaombe abiria kutimiza matakwa ya kisheria, kwani watu wamekuwa
wakifanya makosa bila kujua sheria,” amesema.
No comments:
Post a Comment