Na Mwandishi wetu
IMEELEZWA kuwa kuna umuhimu wa kutoa taarifa kwa
wananchi zinazohusu utekekezaji wa miradi ya maendeleo.
Wakizungumza katika mkutano wa kuandaa taarifa kwa
wadau wa maji katika kata za Kwembe, Msigani na Kibamba, washiriki wamesema sheria na taratibu zilizo wekwa taarifa ni muhimu ili
wananchi wawe na mrejesho wa miradi inayowahusu.
Mwezeshaji wa mkutano huo ulioandaliwa na Asasi ya Pakacha na kufadhiliwa na The Foundation For Civil Society,
Bumija Moses amesema wananchi wanaweza kuleta msukumo wa kiutendaji kwa
viongozi kama wakishirikishwa kupata taarifa za miradi inayojengwa na utekelezaji
wake.
Mkutano huo ulikutanisha wananchi na viongozi kutoka
katika katika kata tatu za Kwembe, Msigani na Kibamba.
Mkutano huo ulifanyika Ijumaa mjini Kibaha.
Diwani wa viti maalumu (Chadema) wa kata ya
Msigani,mheshimiwa Vicky Mchome amesema ushirikishwaji wa wananchi katika
sehemu nyingi, ikiwemo kata yake haupo akitoa wito kwa wananchi
kupewa taarifa.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kwembe, Peter Chawala
amesema wananchi wasisubiri kushirikishwa, wana haki ya kuuliza
viongozi wao ili kupata taarifa zinazowahusu.
Adam Kingu, mkazi wa Maramba Mawili amesema licha ya
wananchi, wapo
pia baadhi ya viongozi ambao hawapati taarifa za
utelekezaji wa miradi ya Maji.
“Unaweza kwenda kumuuliza mtendaji lakini cha
kushangaza hajui bajeti iliyotengwa au hata mradi unaotekelezwa”, amesema
Kingu.
Kata za Kwembe, Msigani na Kibamba zina changamoto za
upatikanaji wa maji, hivyo kupelekea Pakacha kuunda kamati maalumu
iliyowashirikisha wananchi na kupita katika kata zote ili kujua kuna
miradi ipi ya maji iliyotengewa bajeti na hatua iliyofikia katika
utekelezaji wake.
Mmoja wa mjumbe wa kamati hiyo, Almas Mohamed amesema
wamepata malalamiko mengi ya wananchi kutojua utekelezaji wa
miradi ya maji iliyopo katika kata zao.
Miongoni ya miradi hiyo ni ujenzi wa kisima cha maji
cha Kibamba kilichotengewa milioni 280 kwa utekelezaji wa kuanzia
mwezi April mwaka jana mpaka june mwaka huu na ujenzi wa tanki la
maji lililopo Kwembe Kingazi B uliotengewa milioni 55, ukiwa katika hatua za mwisho.
Katibu wa Pakacha, Haroun Jongo amesema serikali inafanya
jitihada kubwa kuleta maendeleo kwa wananchi, ndio maana asasi
kama Pakacha zinapata fursa ya kuelimisha wananchi.
“lengo la mkutano huo ni kuandaa taarifa kwa
kuwashirikisha wananchi, baada ya kufanya upembuzi yakinifu ya miradi iliyopo.
No comments:
Post a Comment