PRESS RELEASE
Wateja wa
Tigo kupata faida mara tatu kupitia promosheni za kusisimua
Mtwara, Oktoba
13, 2018 – Huku msimu wa mavuno ya
korosho ukiwa umewadia katika mikoa ya nyanda za juu kusini, wakaazi wa Mtwara
na viunga vyake wanajiandaa kuvuna vibe kama lote kutoka kwa mastaa wa muziki
wa bongo flava katika msimu unaoendelea wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote.
Mkuu
wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa {Katikati} akiongea na waandishi wa Habari kuhusiana na fursa mbalimbali za kibiashara zinatazopatika
katika mkoa huo kutokana na ujio wa tamasha la Tigo Fiesta 2018 - Vibe Kama
Lote linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii katika viwanja vya Nangwanda Sijaona. Kushoto kwake ni
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa na Mratibu wa Tamasha la
Tigo Fiesta, Pancras Mayalla {maarufu kama Askofu TZA}.
Waandaaji Clouds Media Group, kupitia Katibu
Kiongozi wa Kamati ya Maandalizi, Gardner Habash amewaalika wakaazi wa Mtwara
waje kupumzika baada ya shughuli ngumu za kuvuna korosho kwa kusikiliza 100%
vibe za nyumbani.
‘Kwa wafanyabiashara, msimu waTigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ni
fursa ya kujiongezea kipato kwa kutoa huduma za usafiri, malazi, vinywaji na
chakula na huduma nyingenezo zinazohitajika na maelefu ya mashabiki
watakaojitokeza kushuhudia tamasha hili,’ Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius
Byanakwa alisema.
Kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Supa Nyota,
wasanii wanaochipuka kutoka Mtwara watapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao, na
wale watakaofanya vizuri watapewa fursa ya kutumbuiza katika tamasha kuu la
Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote linalotarajiwa kurindima siku ya Jumapili
tarehe 14 Oktoba katika viwanja vya Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
‘Mbali na
muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi mara mbili ya thamani kwa
vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia *147*00#.
Mkurugenzi
wa Tigo Kanda ya Pwani, Joseph
Mutalemwa (Kulia) akiwa na Mkuu wa Mkoa
wa Mtwara, Gelasius Byakanwa (katikati) pamoja na Mratibu wa Tigo Fiesta 2918 ,
Pancras Mayalla katika Mkutano na waandishi wa habari
kueleza maandalizi ya tamasha la Tigo Fiesta 2018 litakalofanyika Uwanja wa
Nang'wanda Jumapili hii pamoja na ofa mbalimbali za Kampuni ya Tigo katika
msimu huu ikiwemo mfumo wa malipo kwa
wakulima wa korosho kupitia huduma za Tigo Pesa.
Promosheni ya Data
Kama Lote itahakikisha kuwa mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio
yote ya msimu wa Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi
kwenye mtandao wenye kasi zaidi wa 4G+,’ Mkurugenzi wa Tigo, Kanda ya Pwani Joseph
Mutalemwa alisema.
Wateja wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10
millioni, zawadi za kila wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH
100,000 kwa kushiriki katika shindano la Tigo
Fiesta 2018 – Chemsha Bongo.
Ushiriki katika shindano hilo unapatikana kwa
kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz.
Watakaoshusha vibe kama lote mjini Mtwara ni pamoja
na kundi la Rostam (Roma and Stamina), Fid Q, Zaid na Weusii (Joh Makini, Niki
wa Pili na G-Nako) ambao walikonga mioyo ya wapenzi wa muziki mjini Iringa.
Wengine ni wasanii a bongo flava Mesen Selekta na Foby, wakongwe Chegge, Barnaba
na Mr Blue, pamoja na akina dada Ruby na Lulu Diva.
TIketi za Tigo Fiesta 2018 – Mtwara zinapatikana
kwa bei punguzo ya TSH 5,000 kupitia Tigo Pesa Masterpass QR kwa kupiga *150*01#, kuchagua namba 5 (lipia
bidhaa), na kuchagua namba 2 (lipa kwa Masterpass). Tuma kiasi husika cha TSH 5,000 kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.
Tamasha la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote tayari
limezuru mikoa ya Morogoro, Sumbawanga na Iringa, na linatarajiwa kutembelea
mikoa ya Singida, Songea, Moshi, Tanga,
Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku fainali ikiwa Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment