Na Mwandishi Wetu
MAMLAKA ya Viwanja vya Ndege imetoa msaada wa mafuta
kwa wanafunzi walemavu wa ngozi wa shule za msingi za Uhuru Mchanganyiko na ile
ya Jeshi la Wokovu jijini Dar es Salaam.
Jumla ya chupa 55 za mafuta hayo ya ngozi aina ya
Infinity Care SPF 30 Sun Screen, ambapo kichupa kimoja kina gharama ya Sh
25,000 na kufanya gharama yote kuwa ni Sh 1,375,000.
Akikabidhi mafuta hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Richard Mayongela, mwakilishi huyo
Naomi Semadio alimkabidhi kila mwanafunzi kichupa cha mafuta hayo kwa ajili ya
matumizi ya kila siku.
Alisema kuwa hatua hiyo ya TAA ya kutoa msaada huo ni
sehemu ya kawaida ya sera ya mamlaka hiyo kusaidia jamii kwa kutatua matatizo
yake, ambapo kwa vijana hao, changamoto kubwa kwao ni matatizo ya ngozi.
Alisema wamekuwa wakitoa misaada kwa jamii bila
kuwepo kwa ubaguzi wa aina yoyote, ambapo hivi karibuni imefanikisha tamasha la
urithi wetu lililofanyika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam pamoja na kusaidia
Umoja wa Wabunge Wanawake kwa ajili ya kujenga vyoo.
Mwalimu wa shule ya Msingi Jeshi la Wokovu Masoud
Babu aliipongeza TAA kwa msaada huo na kusema kuwa wanafunzi wao albino
wamekuwa na changamoto nyingi ikiwemo hiyo ya tatizo la afya, na hasa ngozi.
Alisema asilimia 70 ya watu wenye alboni wamekuwa wakipoteza
maisha kutokana na saratani ya ngozi, pia alitaka kofia na miwani kwa ajili ya
kuwakinga wanafunzo hayo.
Alisema gharama ya kumtibu mtoto albino ni kubwa na
amewapogeza TAA na kuutumia vizuru msaada huo na amewataka wasiwasahau,
waendelee kuwasaidia.
“Msaada huu utakuwa ni mwanzo kwani wanatarajia TAA
itaendelea kuwasaidia kwa masuala mbalimbali, hasa ukizingatia mafuta hayo yana
gharama kubwa na wengi wanashindwa kumudu gharama zake, “alisema mwalimu huyo.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Jeshi la Wokovu, Rehema
Mwahalende alishukuru TAA kwa msaada huo kwani utawasaidia wanafunzi hao
kuepukana na matatizo ya ngozi, ambayo yanasababisha saratani.
Alisema TAA imeonesha mfano wa kuigwa kwa kuwajali
watoto hao na wanatarajia wataendelea kuwasaidia katika nyanja mbalimbali.
No comments:
Post a Comment