Wednesday, 14 October 2015

Hafla ya Taswa kumuaga Kikwete na kumkabidhi tuzo ya kuendeleza michezo nchini

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa), Juma Pinto (wa pili kulia), akimkabidhi rais Jakaya Kikwete tuzo maalum ya kuendeleza michezo nchini katika kipindi chake cha uongozi cha miaka 10. Pia hafla hiyo ilikuwa maalum kwa ajili ya kumuaga na kumuwezesha yeye (Rais) kutoa tuzo kwa wanamichezo 10 waliofanya vizuri katika kipindi chake hicho cha miaka 10.
Kipa wazamani wa Simba na Taifa Stars, Mohamed Mwameja (katikati), akiteta na Mtangazaji wa E.FM, Maulid Kitenge wakati wa hafla ya Taswa. Kulia ni mpiga picha wa kujitegemea, Makongoro.

Mwanariadha wazamani wa mbio fupi nchini, Peter Mwita (kulia), akizungumza na mwanariadha wazamani wa marathoni aliyepata mafanikio makubwa katika mbio mbalimbali kubwa za umbali huo na Katibu Mkuu wazamani wa kilichokuwa Chama cha Riadha Tanzania (TAAA), sasa Riadha Tanzania (RT), Juma Ikangaa wakiwa pamoja na mdau wa michezo.

Waandishi wa habari Salehe Ally (kushoto) akiwa na baadhi ya viongozi wa Taswa, Shija Richard (kulia), Grace Hoka na Egbert Mkoko wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza hafla ya Taswa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mchezaji wazamani wa mpira wa kikapu nchini na mwandishi wa Azam TV, Patrick Nyembera akizungumza na mwenyekiti wazamani wa Chama cha Netiboli Tanzania, Anna Bayi. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi.

Peter Mwita akisalimia na kiongozi wazamani na mwamuzi wa ndondi Mutta (kulia), huku aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha Ndondi Tanzania, Alhaj Shaaban Mintanga akishuhudia.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Saleh Zonga (kulia), akiteta na kocha wazamani wa timu ya mpira wa kikapu ya ABC, Martine Kemwaga. Katikati ni Manase Zablon.
Saleh Zonga (kulia) akiteta na Martine Kemwaga katika hafla ya Taswa.
Mwandishi Mwandamizi nchini, Peter Mwenda (kulia) akisalimiana na mwenyekiti wazamani wa Chama cha Ndondi Tanzania, Shaaban Mintanga katika hafla ya Taswa.

No comments:

Post a Comment