Wednesday 14 October 2015

Van Persie ajifunga wakati Uholanzi ikikwama kufuzu kwa Euro 2016


Mchezaji wa timu ya taifa ya Uholanzi, Robin van Persie akijifunika uso baada ya kujifunga timu yake ilipocheza na Jamhuri ya Czech.
TERDAM, Uholanzi
MBIO za Uholanzi kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Ulaya za Euro 2016 zilifikia kikomo juzi, wakati Robin van Persie akijifunga wakati timu hiyo ikipata kipigo katika mchezo wa nyumbani dhidi ya Jamhuri ya Czech iliyokuwa na wachezaji 10.

Timu hiyo ya Uholanzi ilihitaji ushindi huku Iceland ilitakiwa kuifunga Uturuki kupata nafasi ya kucheza mchezo wa marudiano, lakini makosa ya Van Persie yaliifanya timu hiyo ikifungwa 3-0 licha ya Mark Suchy kupewa kadi nyekundu.

Klaas-Jan Huntelaar na Van Persie walijibu kutoka katika mabao ya Pavel Kaderabek na Josef Sural lakini badala yake ilikuwa Uturuki ndio iliyochukua nafasi ya tatu.
Timu ya Fatih Terim iliifunga Iceland 1-0.
 
Turkey Ilifuzu
Uturuki ilishuhudia mchezaji wake Gokhan Tore akitolewa nje katika dakika ya 78 wakati mchezo wake ukionekana kuwa sare, lakini bao la dakika za mwisho la Selcuk Inan liliwafanya kuibuka na ushindi.

Matokeo hayo yana maana kuwa Uturuki imefuzu kwa fainali zijazo za Ulaya zitakazofanyika Ufaransa mwakani.

Ukraine na Norway zote zilimaliza katika nafasi ya tatu kutoka katika makundi yao na zina pointi zaidi ya Uturuki.

Kocha wa Uholanzi Danny Blind aliyeanza kuifundisha timu hiyo Julai akichukua nafasi ya mtangulizi wake Guus Hiddink aliyeondoka baada ya miezi 10 katika nafasi hiyo.

Alipoteza mechi tatu kati ya nne akiifundisha timu hiyo lakini amesema kuwa hana mpango wa kuachia ngazi.

"Nitaendelea kufanyakazi yangu kwasababu niko katika mkataba hadi mwaka 2018 na ninaamini katika timu hii," alisema Blind.
 
Uholanzi, iliyomaliza ya tatu katika fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil, ilitwaa taji la Ulaya mwaka 1988 huku ikimaliza ya tatu mwaka 1992, 2000 na 2004.

Kwa mara ya mwisho ilishindwa kufuzu kwa mashindano makubwa mwaka 2002 zikiwa ni fainali za Kombe la Dunia, ambako walitolewa kutoka katika mashindano ya mwaka 1982 na 1986 na kutokakatika mashindano ya Ulaya mwaka 1984.

No comments:

Post a Comment