Sunday, 11 October 2015

Blatter, Platin huenda wakafungiwa maisha kujihusisha na soka



 ZURICH, Uswisi
SEPP Blatter na Michel Platini huenda wakajikuta wakitupwa nje ya soka kwa miaka kadhaa kutokana na kupatikana kwa ushahidi mpya kuhusu matumizi mabaya ya fedha yaliyoibuliwa na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa).

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya kamati hiyo ya maadili kilisema kuwa kamati hiyo ilibaini uozo huo siku chache zilizopita na huenda ukasababisha wawili hao kuondolewa katika soka kwa miaka kadhaa, imebainika.

Endapo hilo litathibitishwa, basi miaka 17 ya Blatter katika uraisi wa Fifa atapigwa `stop kujihusisha na soka maisha, wakati hatma ya Platini katika siasa za soka itakuwa imeharibiwa kabisa.

‘Kwa sasa jazba ni kubwa sana lakini hili liko vibaya sana tofauti na wengi wanavyofikiria, ‘ kilisema chanzo hicho kikubwa kilicho karibu sana na kamati hiyo ya maadili.

Blatter na Platini walifungiwa kwa takribani siku 90 wakati Kamati ya Maadili ikichunguza malipo yanayodaiwa sio halali ya kiasi cha pauni milioni 1.3 kwa Platini, yaliyoidhinishwa na Blatter, mwaka 2011.

Wote wawili wanasisitiza kuwa hawana hatia. Platini anataka kifungo chake hicho kiondolewa kupitia rufaa iliyokatwa  na Chama cha Soka cha Ufaransa katika Mahakama ya Usuluhishi wa mambi ya Michezo (CAS).
Endapo rufaa hiyo itashinda, basi Platin anawea kuwania kiti cha urais wa Fifa ili kumbadili Blatter kabla ya siku ya mwisho ya kuwasilisha fomu ya kutaka kugombea Oktoba 26.

Hatahivyo, hadi sasa bado haijajulikana kama uchaguzi wa Februaria kama utafanyika kama ulivyopangwa.

No comments:

Post a Comment