Muimbaji Nassib Abdul au Diamond akiimba wakati wakati wa mazoezi kwenye ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya kutumbuiza na Wizkid wa Nigeria Jumamosi. |
Na Mwandishi Wetu
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya Nassib Abdul, Diamond Platinum ataimba jukwaa moja na
msanii mahiri kutoka Nigeria, Wizkid katika tamasha litakalofanyika katika
viwanja vya Leaders Kinondoni Jumamosi.
Akizungumza
na waandishi wa habari mratibu wa onesho hilo, Solomon Nassuma alisema kuwa, msanii
huyo atawasili Ijumaa mchana tayari kwa shoo hiyo.
Alisema
kuwa tiketi za viti maalum ndio zimeshaanza kuuzwa katika vituo mbalimbali kama
vile katika migahawa yote ya Eaters Points iliyopo Oysterbay na Namanga,
Onetash, migahawa yote ya KFC pamoja na hotel ya Rainbow Mbezi.
Aliongeza
kuwa kwa wale watakaokata viti maalum kutakuwa na magari kwa ajili kuwachukua
kutoka maeneo mbalimbali ambapo watakuwa wameegesha magari yao.
Alisema
kuwa maeneo hayo ni katika eneo la ukumbi wa King Solomon Hall na mgahawa wa
Eaters point Oysterbay yatawabeba na kuwapeleka moja kwa moja ukumbini na kisha
kuwarudisha tena kwenye magari yao baada ya kumalizika kwa onesho.
"Hii
inatokana na ukweli kwamba hawa watu wa VIP tunataka wafurahie fedha zao za
kiingilio kwa kuwa wamekata fedha kubwa na inatakiwa kuhakikisha kuwa
wanafurahia shoo pia" alisema Nassuma.
Aliongeza:
"Kwa tiketi nyingine za kawaida zitaanza kuuzwa siku hiyo hiyo ya shoo na
naomba wananchi mbalimbali kujitokeza kushuhudia kwani tayari zoezi la Uchaguzi
Mkuu lilishamalizika.”
Aliongeza
kuwa pia watakuwa wasanii wengine kama vile Christian Bella pamoja na Farid
Kubanda, Fid Q na wengine.
Baadhi ya madansa wa Diamond wakifanya mazoezi katika ukumbi wa King Solomon jana kwa ajili ya onesho la Jumamosi. |
"Hii
inakuwa ni shoo ya kwanza ya Diamond tangia ashinde tuzo hizo na kwanza inakuwa
ni shoo ya live sasa hayo ni mafanikio makubwa na wananchi wataona shoo hiyo
wakati wakiwa ndio kwanza wametoka kwenye uchaguzi mkuu" alisema Tale.
Diamond
ambae kwa sasa ni mmoja kati ya wasanii wakubwa barani Afrika ambapo ameshinda
tuzo ya msanii bora wa Afrika Mashariki na Afrika katika tuzo za Afrima
zilizofanyika Marekani huku akiwa pia ni mshindi wa tuzo ya msanii bora wa
Afrika ya MTV EMA.
No comments:
Post a Comment