Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa
Anga Tanzania (TCAA), Hamza Johari (mbele), leo
kwenye ukumbi wa Watu Mashuhuri wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha
Julius Nyerere (JNIA-TBII), akifungua mkutano wa siku tatu wa Wataalam wa Usafiri
wa Anga WA Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambao wanajadili namna ya kuboresha
huduma na miundombinu ya usafiri huo kwa nchi wanachama. Mkutano huo
unashirikisha wajumbe zaidi ya 90.
Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha (aliyesimama kushoto) akiwasilisha maelezo yanayohusu majengo matatu
ya abiria ya Kiwanja hicho kwa Wataalam wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki, leo wameanza mkutano wa siku tatu wa kujadili namna ya kuboresha huduma
na miundombinu ya usafiri huo kwa nchi wanachama.
Wataalam wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki, ambao wapo nchini kushiriki mkutano wa siku tatu wa kujadili
namna bora ya kuboresha huduma na miundombinu ya usafiri huo, ambapo leo
wametembelea majengo ya mizigo yaliyopo kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa
cha Julius Nyerere (JNIA).
No comments:
Post a Comment