Na
Bahati Mollel,TAA
VIWANJA
vya Ndege Tanzania sasa vinaweza kutumika majira yote ya mwaka ya masika na
kiangazi kutokana vingi barabara zake za kutua na kuruka ndege kujengwa kwa
kiwango cha lami, imeelezwa.
Mkurugenzi
wa Idara ya Uhandisi na Huduma za Ufundi, Mhandisi Mbila Mdemu ametoa maelezo
hayo leo kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),
alipozungumza na Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini,
wakati alipozungumzia mafanikio ya Mamlaka hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya
Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Viwanja
hivyo ni Arusha, Tabora, Mwanza, Bukoba, Mafia, Iringa, Songwe, Tanga, Moshi,
Songwe, Kigoma, Dodoma, Mtwara, Mpanda pamoja Viwanja vya Ndege vya Kimataifa
vya Julius Nyerere (JNIA) na Kilimanjaro (KIA).
“Tangu
kuanzishwa Mamlaka vilikuwepo viwanja nane pekee vyenye viwango vya lami,
lakini sasa mpaka Novemba mwaka 2015 tumeweza kuongeza na kufikisha 16 ambavyo
vinapitika kwa uhakika zaidi katika majira yote ya mwaka ya kiangazi na
masika,” amesema Mhandisi Mdemu.
Mbali
na barabara za kutua na kuruka ndege, pia Mamlaka hiyo imefanikiwa kufanya ukarabati
na upanuzi wa majengo ya abiria na kufanikisha kuweza kuhudumia abiria wengi
zaidi ya wa awali, ambapo ni pamoja na jengo la tatu la abiria la JNIA, Bukoba,
Dodoma, Iringa, Mpanda, Mtwara na Mwanza.
Pia
Mhandisi Mdemu amesema mafanikio mengine ni kuboresha ulinzi wa kutosha wa
abiria na mizigo, kwa kufungwa kamera za kufuatilia matukio, kuwepo kwa mashine
za kukagua abiria na mizigo na kujengwa kwa uzio kwenye baadhi ya viwanja,; pia
kumefungwa mifumo ya kisasa ya kiyoyozi; na kuanza kusimikwa kwa taa za kuongoza ndege ili
ziweze kutua usiku.
Naye
Meneja Mipango na Takwimu wa TAA, Asteria Mushi amesema kuwa Mamlaka imeweza
kupata mafanikio kwa kuongeza mapato kutoka Tshs. Bil. 63 kwa mwaka 2015 na
kufikia Bil. 105 kwa mwaka 2018, ambazo ni ongezeko la asilimia 66, ambapo
lengo la Mamlaka ni kuongeza mapato na kufikia Tshs. Bil. 130 ifikapo mwaka
2020; pia wameweza kuongeza biashara za maduka na sasa serikali wanashirikiana
na taasisi binafsi kujenga hoteli ya nyota nne yenye ghorofa nane (8) itakayojengwa
karibu na jengo la pili la abiria (JNIA-TBII).
Hali
kadhalika Mushi, amesema Mamlaka imeongeza idadi ya ndege za abiria ambazo
awali zilikuwa zikifanya safari nchini, lakini baadaye zikasitisha na zimeanza
tena safari hizo, ambazo ni Air Uganda na Zimbabwe. Ndege hizo zinafanya idadi
ya ndege za nje kufikia 21.
“Katika
viwanja vya ndege tumetenga asilimia 30 kwenye majengo ya abiria tumetenga
huduma za abiria na biashara, lakini tunaangalia na ongezeko la ndege za Air
Tanzania ambapo sasa zinakwenda njia 10 za ndani ya nchi na njia tano za
kimataifa,” amesema Mushi.
No comments:
Post a Comment