Na Mwandishi
Wetu
KAMPUNI ya
Simu za Mkononi ya Tigo itapeleka mashabiki 10 wa soka kuishangilia timu ya
taifa ya Tanzania, Taifa Stars, katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya
Afrika, Afcon 2019, nchini Misri, imeelezwa.
Taifa Stars, itashiriki
kwa mara ya kwanza fainali hizo baada ya kushiriki mara ya mwisho miaka 39
iliyopita, wakati mashindano hayo yalipofanyikia Lagos, Nigeria mwaka 1980 na
tangu wakati huo imekuwa ikiishia katika hatua ya kufuzu.
Tigo
wameanzisha promosheni ya Soka la Afrika ili kupata kupata watu 10, ambao mbali
na kujishindia nafasi hizo za kwenda kuishangilia Taifa Stars ikicheza Afcon
2019, pia watapata nafasi ya kuwa mamilionea.
Akizungumza na
waandishi wa habari katika uzinduzi wa Soka la Afrika jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa Bidhaa na Huduma wa kampuni hiyo, David Umoh alisema kuwa wateja
wa Tigo wanayo nafasi ya kujishindia safari ya kwenda Misri kushuhudia Kombe la
Mataifa ya Afrika pamoja na zawadi za fedha taslimu.
Kampuni hiyo
imetenga zaidi ya Sh Milioni 50 katika promosheni hiyo ya Soka Letu, ambapo pia
kutakuwa na washindi 10, ambao watagharimiwa kila kitu kwenda kuishuhudia Taifa
Stars katika michuano hiyo ya Afcon 2019.
“Tunaamini kwa
kutumia mashindano haya, tunaweza kupata fursa nzuri kutoa habari, elimu na
burudani kwa kutumia jukwaa la mawasiliano na huduma za kampuni hiyo katika
kutumia huduma na bidhaa zetu, “alisema Umoh.
Fainali za
Afcon ni mashindano makubwa kabisa barani Afrika kwa timu za taifa, ambazo
zinawaleta pamoja wachezaji wa Kiafrika wanaoshiriki ligi kubwa na zenye
ushindani ndani na nje ya Afrika.
“Tunaamini
itakuwa jambo zuri kwa wateja wetu kupata nafasi ya kwenda kushuhudia
mashindano haya makubwa ikiwa ni pamoja na kushangilia timu yetu ya Taifa Stars
itakayotuwakilisha. Tunawatakia kila la kheri, “aliongeza Umoh.
Alisema zaidi
ya wateja 100 watashinda zawasi za fedha taslimu kila siku, wiki na kila mwezi
kwa muda wa miezi mitatu katika shindano hilo, ambalo mshiriki atatakiwa kutuma
neno SOKA kwenda 15670 ili kuweza kujibu maswali yanayohusu Afcon 2019.
Mashindano ya 32
ya Afcon 2019 yataanza Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 19 na Tanzania
imepangwa Kundi C pamoja na Kenya, Senegal na Algeria na itaanza kampeni zake
kwa kucheza dhidi ya Senegal.
No comments:
Post a Comment