1.
Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni ya
MultiChoice Tanzania Balozi Ami Mpungwe {Kulia} sambamba na Mkurugenzi Mtendaji
wa kampuni ya Jacqueline Woiso , akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa
kampeni hiyo maalum ya Afcon 2019 ijulikanayo kama “DStv Tupogo”.
Na Mwandishi Wetu
HUKU zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, Afcon 2019, Misri, Kampuni ya MultiChoice
Tanzania (DStv) imetangaza rasmi kampeni maalumu kwa Watanzania
itakayowawezesha kushuhudia michezo yote 52 ya mashindano ya Kombe hilo mubashara kupitia chaneli za Supersport zilizo katika mfumo wa HD.
Akizungumza katika hafla ya kuzindua
kampeni hiyo ya DStv ijulikanayo kama ‘DStv Tupogo’ hivi karibuni, Mkurugenzi
Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Jacqueline Woiso amesema wana furaha kubwa kupata fursa hiyo.
“Tuna furaha
kubwa kwa nchi yetu kupata fursa ya kushiriki katika michuano hii ya kimataifa
baada ya takribani miaka 39 toka iliposhiriki kwa mara ya mwisho mnamo mwaka 1980. Na kama ilivyo ada, ni jukumu letu na la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa
tunawatia moyo vijana wetu na kuifanya nchi yetu ifanye vizuri katika michuano
hii ya kimataifa.
1.
Baadhi ya wachambuzi wa Kiswahili wa
Supersport wakiwa katika picha ya pamoja
wakati wa utambulisho wa mchambuzi mpya mwadada Salama Jabir.
Kwa kuzingatia hilo DStv imehakikisha
kuwa mechi zote 52 za michauano hii ya kimataifa ya Afcon 2019 itarushwa mubashara
DStv kupitia chaneli za Supersport na kwa lugha adhimu ya Kiswahili na katika mfumo wa HD.
Zaidi ya hayo, DStv
imehakikisha kuwa mechi hizo zinaonekana katika vifurushi vyote kuanzia kile
cha DStv Bomba cha Sh. 19,000 tu. “Tumehakikisha
kuwa mechi hizi zinakuwepo hadi kwenye kifurushi cha chini kabisa ili
kuwawezesha watanzania wengi kushuhudia mtanange huo na kuwa sehemu ya historia
ya nchi yetu kwani tunashiriki baada ya zaidi ya miaka 30”, alisema Jacqueline.
Sambamba na uzinduzi huo pia ulifanyika
utambulisho wa wachambuzi wa Kiswahili wa Supersport, ambapo kwa mara ya kwanza
mwanadada Salama Jabir ataungana na timu hiyo katika kuongeza ladha na vionjo
na hivyo kuongeza burudani na msisimko wa watazamaji. Wenginde ni wachambuzi
mahairi akiwemo Aboubakar Liongo, Ibrahim Maestro, Edo Kumwembe, Maulid Kitenge
pamoja na Oscar Oscar.
1. Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Dk Yussuf Singo akizungumza
wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni maalum ya Afcon 2019 ya “DStv Tupogo”.
1.
Baadhi ya wachezaji wa zamani timu ya
Taifa walioshiriki katika mashindano ya Afcon 1980, wakiwa katika picha ya
pamoja na Mkurugenzi na Maendeleo ya Michezo wizara Dk Omar Singo sambamba na Mwenyekiti wa Bodi
ya Kampuni ya Multihoice Tanzania, Balozi Ami Mpungwe na Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni hiyo, Jacqueline Woiso.
Akiongea katika uzinduzi wa kampeni hiyo
ya Tupogo Hussein Ngulungu moja kati ya wachezaji nguli waliowahi kushiriki
katika michuano ya Afcon 1980, alisema kuwa, “Kwa mara ya kwanza baada ya
takribani miongo minne, Tanzania imepata tena heshima kubwa ya kushiriki katika mashindano
haya makubwa hivyo ni wajibu wetu sisi watanzania kuonyesha uzalendo na kuwatia
moyo vijana wetu ili kuhakikisha wanafanya vyema katika michuano hii ili kuipatia
sifa nchi yetu“ alisema Hussein.
Mbali na michuano ya Kombe la Afcon 2019
itakayoanza hivi karibuni, wateja wa DStv pia wataendelea kufurahia maudhui
mbalimbali zikiwemo sinema na tamthilia mbalimbali kutoka nje na hapa nyumbani
kama vile msimu mpya wa vichekesho vya Kitimtim, tamthilia ya HUBA, Rebeca
kipindi maarufu cha Shilawadu Xtra na bila kusahau cha Maisha Yangu
kinachoelezea maisha na mapito ya watu mashuhuri kutoka hapa nyumbani Tanzania
vyote vikiwa vinapatikana kupitia chaneli ya Maisha Magic Bongo iliyopo katika
kifurushi cha Bomba.
No comments:
Post a Comment