Sunday 16 June 2019

Mbwana Samatta Atakiwa Lazio Kwa Bilioni 41.2


ROME, Italia
NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, na mshambuliaji wa Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta ni mmoja mwa wachezaji waliotangazwa hivi karibuni kabisa kusakwa na Lazio kwa ajili ya usajili wa kipindi hiki cha majira ya joto.

Samatta alifunga mabao 20 katika mechi 28 alizocheza katika Ligi Kuu ya Ubegiji msimu uliopita, huku akisaidia mara tatu. Baada ya kusaini Genk akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ada ya uhamisho na kiasi cha sh bilioni 2, Samatta sasa ana thamani ya zaidi ya sh bilioni 30 na Lazio wako tayari kumchukua kwa sh bilioni 41.2.

Mkataba wa Samatta Genk unamalizika mwakani na itakuwa kazi kubwa kumchukua mchezaji huyo kumpeleka Rome katika kipindi hiki cha majira ya joto.

Lazio ni klabu ya Italia yenye maskani yake jijini Rome nchini humo, na inajulikana sana kwa shughuli zake za soka katika eneo hilo na inashiriki katika Ligi Kuu ya Italia ya Serie A.

Lazio imewahi kutwa taji la Ligi Kuu ya Italia mara mbili (mwaka 1974 na 2000), na wamewahi kushinda taji la Coppa Italia mara saba na mara nne lile la Supercoppa Italiana, na wamewahi kuwa mabingwa wa Kombe la Ligi ya Mabingwa pamoja na lile la Super Cup katika wakati mmoja.

Klabu kadhaa zinazoshiriki Ligi Kuu ya England, ikiwemo West Ham tayari zimeonesha nia ya kutaka kumsajili mchezaji huyo wazamani wa Simba na TP Mazembe.


No comments:

Post a Comment