Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issac Kamwelwe leo akifungua
Jukwaa la Pili la Kitaifa la Usafiri wa Anga linalofanyika kwa siku mbili
kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini
Dar es Salaam.
Na
Mwandishi Wetu
SERIKALI
imesema imeweka mipango kabambe ya kuboresha viwanja vidogo vya ndege (Airstrips),
ili viweze kutumika kirahisi na ndege ndogo zinazosafirisha Watalii kutembelea
mbuga mbalimbali za wanyama na vivutio vilivyopo nchini.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Issac
Kamwelwe katika Jukwaa la Pili la Kitaifa la Usafiri wa Anga linaloendelea
kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), ambapo
tayari imeundwa kamati kutembelea viwanja hivyo, ambavyo amesema vipo zaidi ya
600 vikiwemo vya makampuni binafsi.
“Hivi
viwanja ndivyo vinavyoingiza Watalii ndani ya mbuga na vivutio vingine baada ya
kushuka pale KIA (Kilimanjaro International Airport) na hapa Dar es Salaam
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), sasa hivi vinatakiwa
viwe katika ubora mzuri utakaofanya Watalii kujiona wapo sehemu nzuri na salama,”
amesisitiza Mhandisi Kamwelwe.
Wadau
mbalimbali wa masuala ya usafiri wa anga leo kwenye Kituo cha Kimataifa
cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC),
wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi wa Jukwaa la Pili la
Kitaifa la Usafiri wa Anga, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,
Mhandisi Issac Kamwelwe.
Hata
hivyo, Mhandisi Kamwelwe amesema Idara ya Uhandisi ya Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA), itaimarishwa zaidi ili iweze kufanya marekebisho kwenye
viwanja hivi, ikiwezekana kununuliwa vifaa ili kufanya kazi kwa ufanisi.
Pia
amesema tayari Serikali imeweza kusimamia vyema mradi wa ujenzi wa Jengo la
Tatu la abiria la JNIA, ambao umekamilika na limeongeza uwezo wa kuhudumia
abiria, ambapo itahudumia abiria milioni sita kwa mwaka badala ya milioni 2 waliokuwa wakihudumia na Terminal 2.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),
Vedastus Fabian (kushoto) akiwasikiliza Maafisa Naomi Mbilinyi na Gladston
Mlay (kulia), kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), katika maonesho
yanayokwenda sambamba na Jukwaa la Pili la Kimataifa la Usafiri wa Anga
linalofanyika kwa siku mbili mfululizo kwenye Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).
“Ninawataka
wafanyabiashara na wadau wengine wote kuchangamkia fursa za kibiashara zilizopo
kwenye jengo letu hili la kisasa, ambapo sasa nimetaarifiwa wapo katika hatua
za kuwapata watoa huduma ndio maana ninasema mjitokeze kwa wingi kuomba,”
amesema Mhandisi Kamwelwe.
Dkt
Bartholomew Rufunjo (kulia) leo akipata maelezo mbalimbali kuhusiana na
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kutoka kwa Mhandisi Astelius
John (kushoto), kwenye maonesho yanayokwenda sambamba na Jukwaa la Pili la
Kitaifa la Usafiri wa Anga yanayofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC). Wengine pichani ni Afisa Masoko wa
TAA, Pendo Mwakilasa akizungumza na Mtendaji Mkuu wa VIA Aviation Ltd, Suzan
Mashibe.
Akizungumzia
viwanja vingine amesema baada ya kukamilika kwa upanuzi na ukarabati wa viwanja
vya ndege vya Songwe na Mwanza vitawekwa katika daraja la Kimataifa, kutokana
na kuwa na miundombinu ya kisasa, ambapo kwa upande wa Mwanza ujenzi wa jengo
la mizigo upo katika hatua ya mwisho kukamilika.
|
- Mhandisi
Astelius John na Afisa Masoko, Pendo Mwakilasa wa Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (kushoto), leo wakiwaeleza masuala mbalimbali ya viwanja
vya ndege wadau waliotembelea meza ya maonesho yanayokwenda sambamba na
Jukwaa la Pili la Kitaifa la Usafiri wa Anga yanayofanyika kwenye Kituo
cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).
|
Kwa
sasa kiwanja cha ndege cha Songwe kipo daraja 3C na yakikamilika maboresho ya
miundombinu kitakuwa daraja la 4D na Mwanza ni daraja 4C.
No comments:
Post a Comment