Nairobi,
Kenya
MWANASHERIA
wa Kenya ametoa kwa Rais Barack Obama ng’ombe 50 na vitu vingine
vinavyohusiana na mifugo kwa ajili ya mahali ili kumuoa binti wa rais huyo
Malia mwenye umri wa miaka 16, taarifa imeeleza.
Felix
Kiprono alisema alikuwa yuko tayari kutoa ng’ombe 50, kondoo 70 nambuzi 30
ili kukamilisha ndoto yake ya kumuoa binti wa kwanza wa rais huyo kutoka taifa
kubwa zaidi duniani.
"Tangu
mwaka 2008 nilipata nia ya kumuoa Malia, " alisema, katika mahojiano na
gazeti la Nairobi.
Wakati
akipata nia hiyo, Rais Obama ndio kwanza alikuwa katika harakati za kutaka
kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza huku Malia wakati huo akiwa na umri wa miaka
10.
"Ukweli
ni kwamba, toka wakati huo sijawahi kutongoza msichana yeyote na niliahidi kuwa
mwaminifu kwake. Nilishauriana haya na familia yangu na walisema wako tayari
kunisaidia kuongeza mahali, " alisema.
Kiprono
alisema anatarajia kumueleza Obama kuhusu suala hilo na ni matumaini yake kuwa,
rais huyo atakwenda Kenya na binti yake huyo wakati mwezi ujao atakapoitembelea
Kenya kwa mara ya kwanza tangu awe rais wan chi hiyo, nchi ambayo baba yake
alikozaliwa.
Bibi
yake Obama ambaye ni Mkenya, ambaye mapema miaka ya 90, bado anaishi huko Kogelo,
magharibi ya Kenya, ambako kuna ndugu kibao wa rais huyo.
"Kwa
sasa ninaandika barua kwa Obama nikiomuomba aongoxzane na Malia katika zira
yake hiyo ya Kenya. Nategemea ubalozi utawasilisha barua hiyo kwa rais huyo,"
alisema.
Kiprono
alikanusha kuwa anataka kumuoa binti huyo kwa lengo la kufuata utajiri.
"Watu
huenda wakasema naenda katika familia hiyo kwa lengo la kufuata utajiri, pesa
za familia hiyo, lakini hilo sio sababu. Nina mapenzi ya dhati, " alisisitiza.
Mwanasheria
huyo kijana, ambaye umri wake haukuwekwa bayana, alisema tayari ameshapanga mipango
yake ndoa hiyo itafungwa kimila,ambapo shampeni itakuwa ni maziwa ya mtindi,
maarufu kama "mursik".
Kiprono
alisema watakapoowa, yeye na binti huyo wa Obama wataishia maisha ya kawaida
tu.
"Nitamfundisha Malia jinsi ya kukamua ng’ombe maziwa, kupika ugali na
kuandaa vyakula vingine vya kiasili kama mwanamke yeyote mwingine wa Kalenjin
woman," he said.
No comments:
Post a Comment