CAIRO, Misri
BAADA ya kupangwa kwa makundi ya Ligi ya
Mabingwa wa Afrika leo Jumanne, yafuatayo ni maoni ya viongozi na makocha wa
timu zinazoshiriki hatua hiyo wakizungumza ratiba hiyo.
Hatem Abdel Gaafar (Timu Meneja, El Merreikh)
Ratiba ni nzuri na tunatarajia kufanya
vizuri. Hii ni mara yetu ya pili kucheza hatua hii ya makundi. Lengo letu ni
kutwaa ubingwa na hilo tutalifanyia kazi.
Wael Gomaa (Mkurugenzi wa Soka, Al Ahly)
Tulitarajia kupangwa dhidi ya timu ngumu,
kutokana na ushiriki wa klabu zenyewe tangu mwanzo. Karibu klabu 10 angalau
zimewahi kutwaa moja ya mataji ya Afrika huko nyuma.
Hivyo tulijua itakuwa ngumu kwetu kutetea
taji tuliloshinda mwaka jana. Tuna wachezaji wazuri na kocha (Fathi Mabrouk) ambaye
anaijua klabu vizuri sana.
Hamada Anwar (Timu Meneja, Zamalek)
Timu zote zilizofuzu ni mabingwa kutoka
katika nchi zao. Natarajia tutakuwa na matokeo mazuri kutoka katika mchezo wa
kwanza hivyo hatutakuwa katika presha katika mchezo wa marudiano.Tuna msimu
mzuri na tunatarajia kushinda taji hilo.
Frederic Kitengie (Katibu Mkuu, TP Mazembe)
Ni ratiba nzuri kwetu. Katika kundi tuko na
timu mbili zinashiriki kwa mara ya kwanza, ambazo ni Smouha na Moghreb
Tetounae. Hizi zitatusumbua sana kwa sababu ni timu mpya hatuzijui vizuri.
Nimefurahi sana kuikwepa El Merreikh, ambayo
inafundishwa na kocha wetu wazamani Diego Garzitto, ambaye anaijua vizuri timu
yetu. Kundi jingine lina timu za Algeria dhidi ya Merreikh na ni vizuri
tumeliepuka kundi kama hilo.
Mohamed
Ashraf (Rais, Moghreb Tetouane)
Ni vizuri tumezikwepa timu za Algeria. Ratiba
inatupa nafasi angalau kucheza nusu fainali. Tunaangalia mbele kucheza na Smouha,
kufuatia mapokezi mazuri tuliyoyapata wakati tumekwenda Misri kucheza dhidi ya Ahly.
Kwa sasa Sudan, nafikiri El Merreikh ni bora
zaidi ya El Hilal, na hiyo itatuapa sisi nafasi. TP Mazembe ni timu imara sana
katika kundi, lakini tuna nafasi.
No comments:
Post a Comment