SEOUL, Korea ya Kusini
Idara ya Ujasusi ya Korea ya Kusini imesema kuwa Waziri wa Ulinzi
wa Korea Kaskazini ameuawa kwa kutokuwa muaminifu kwa kiongozi wa nchi hiyo,
Kim Jong-un.
Taarifa hiyo iliyotolewa bungeni imesema Hyon Yong-Chol alikutana
na mauti yake baada ya kupigwa kwa kombora la kuangusha ndege mbele ya mamia ya
maafisa wakuu serikalini mwishoni mwa mwezi uliopita.
Bw.Hyon inadaiwa kuwa alisinzia katika hafla iliyokuwa ikihutubiwa
na rais Kim, jambo lililomuudhi sana kiongozi huyo wa kiimla na kuamua kuuawa
kwake hadharani.
Hata hivyo ukweli wa ripoti hiyo haujabainika kutokana na usiri wa
Serikali ya Korea Kaskazini.
Taarifa zingine zinadai kuwa, Waziri wa Ulinzi wa Korea Kaskazini
ameuawa kwa kutokuwa muaminifu kwa kiongozi wa nchi hiyo, Kim Jong-un.
Bw.Hyon alipandishwa cheo na kuwa Generali mwaka wa 2010 na kuuawa
kwake kunatia shaka udhabiti wa uongozi wa rai Kim Jong -un.
Hyon alipandishwa cheo na kutangazwa kuwa waziri wa usalama wa
taifa mwaka uliopita.
Mwandishi wa BBC aliyeko huko Seoul anasema mauaji hayo ya
kikatili mbele ya umma ikiwa yatathibitishwa, yanaonyesha athari za uasi dhidi
ya Kim Jong-un.
Mapema idara hiyo ya ujasusi ilisema viongozi wakuu katika Serikali
ya Korea Kaskazini wamekuwa wakiuawa kila mmoja kwa wiki.
Chang alikamatwa katika mkutano wa hadhara na kupelekwa katika
eneo la hadhara alikouawa.
Mara ya mwisho kwa kiongozi huyo wa Korea Kaskazini kuamrisha
kuuawa kwa kiongozi mkuu serikalini, ilikuwa mwaka 2013 alipoamuru aliyekuwa msaidizi
wake Chang Song auawe
.
Chang alikamatwa katika mkutano wa hadhara na kupelekwa katika
eneo la hadhara alikouawa mbele ya umma.
No comments:
Post a Comment