LONDON, England
KOCHA wa Chelsea Jose Mourinho anasema kuwa
nahodha wa Liverpool Steven Gerrard amemfanya yeye kuwa "kocha bora",
kabla ya timu hizo kukutana Jumapili kwa mara ya mwisho katika msimu huu wa Ligi
Kuu ya England.
Mabingwa hao wapya wa England Jumapili
wanawakaribisha Liverpool katika moja ya mechi za mwisho za Gerrard mwenye umri
wa miaka 34 katika klabu hiyo yenye maskani yake Anfield. Mchezo huo unatarajia
kuanza saa 11:00 jioni.
"Adui yangu, alinifanya kuwa kocha bora
kwa sababu ilikuwa vigumu kumsimamisha, " alisema Mourinho, huku akiongeza
kuwa alijaribu mara tatu kumsajili mchezaji huyo.
"Nasikitika sana hii ni mara ya mwisho
nitakabiliana naye."
Gerrard alikaribia kusaini Chelsea wakati
Mourinho alipoifundisha klabu hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2005, na kocha huyo
Mreno alibainisha kuwa pia alimtaka mchezaji huyo akiwa Inter Milan na hata
alipokuwa akifundisha Real Madrid.
Alisema kuwa amechelewa kumsajili mchezaji
huyo kwa sasa kwani tayari klabu ya LA Galaxy ya Marekani imemuwahi: "Nimechelewa
kumsajili. Hawezi kucheza dhidi ya Liverpool. Amefanya mambo makubwa akiwa
Liverpool. Alikataa kabisa kuchezea klabu nyingine kubwa, ligi nyingine kubwa,
aliamua kuichezea Liverpool pekee.
"Nani alijua kama siku moja nitacheza
dhidi ya Steven kama kocha wa Liverpool?"
Endapo angemshawishi Gerrard kujiunga na the
Blues, Mourinho alisema angekuwa amefanikiwa mchezaji huyo kumchezesha na Frank
Lampard – kitu ambacho
makocha wengi wa England wanadaiwa kushindwa kukifanya.
No comments:
Post a Comment