Friday, 1 December 2017

Makundi, Ratiba Kombe la Dunia 2018 hadharani

MOSCOW, Urusi
WENYEJI Urusi watafungua dimba katika fainali za Kombe la Dunia kwa kucheza na Uswisi katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja mpya wa Luzhniki Juni 14 mwakani.

Kwa mujibu wa ratiba hiyo, wawakilishi wawili wa Afrika, Misri na Morocco wenyewe watacheza siku inayofuata dhidi ya Iran na Uruguay, huku Nigeria ikicheza dhidi ya Croatia Juni 16, 2018.

Kundi A lina timu za Urusi, Saudi Arabia, Uruguay na Misri wakati Kundi B lina timu za Ureno, Hispania, Morocco na Iran.

Kundi C linaundwa na timu za Ufaransa, Australia, Peru na Denmark, huku Kundi D lina timu za Argentina, Iceland, Croatia na Nigeria.

Kundi E: Brazil, Uswisi, Costa Rica na Serbia na Kundi F: Ujerumani, Mexico, Sweden na Afrika Kusini.


Kundi G lina timu za England, Ubelgiji, Tunisia na Panama, Kundi H lina Poland, Senegal, Colombia na Japan.

RATIBA KOMBE LA DUNIA 2018
Thursday 14 June 2018
RussiavSwitzerlandLuzhniki Stadium (new)17:00
Friday 15 June 2018
EgyptvUruguayCentral Stadium Yekaterinburg14:00
MoroccovIranZenit Arena17:00
PortugalvSpainFisht Stadium20:00
Saturday 16 June 2018
FrancevAustraliaKazan Arena12:00
ArgentinavIcelandOtkrytie Arena15:00
PeruvDenmarkMordovia Arena18:00
CroatiavNigeriaKaliningrad Stadium21:00
Sunday 17 June 2018
Costa RicavSerbiaCosmos Arena14:00
GermanyvMexicoLuzhniki Stadium (new)17:00
BrazilvSwitzerlandRostov Arena20:00
Monday 18 June 2018
SwedenvKorea RepublicNizhny Novgorod Stadium14:00
BelgiumvPanamaFisht Stadium17:00
TunisiavEnglandVolgograd Arena20:00
Tuesday 19 June 2018
PolandvSenegalOtkrytie Arena14:00
ColombiavJapanMordovia Arena17:00
RussiavEgyptZenit Arena20:00
Wednesday 20 June 2018
PortugalvMoroccoLuzhniki Stadium (new)14:00
UruguayvSaudi ArabiaRostov Arena17:00
IranvSpainKazan Arena20:00
Thursday 21 June 2018
FrancevPeruCentral Stadium Yekaterinburg14:00
DenmarkvAustraliaCosmos Arena17:00
ArgentinavCroatiaNizhny Novgorod Stadium20:00
Friday 22 June 2018
BrazilvCosta RicaZenit Arena14:00
NigeriavIcelandVolgograd Arena17:00
SerbiavSwitzerlandKaliningrad Stadium20:00
Saturday 23 June 2018
BelgiumvTunisiaOtkrytie Arena14:00
GermanyvSwedenFisht Stadium17:00
Korea RepublicvMexicoRostov Arena20:00
Monday 25 June 2018
Saudi ArabiavEgyptVolgograd Arena16:00
UruguayvRussiaCosmos Arena16:00
IranvPortugalMordovia Arena20:00
SpainvMoroccoKaliningrad Stadium20:00
Tuesday 26 June 2018
DenmarkvFranceLuzhniki Stadium (new)16:00
AustraliavPeruFisht Stadium16:00
IcelandvCroatiaRostov Arena20:00
NigeriavArgentinaZenit Arena20:00
Wednesday 27 June 2018
MexicovSwedenCentral Stadium Yekaterinburg16:00
Korea RepublicvGermanyKazan Arena16:00

Saturday 30 June 2018
TBAvTBAKazan Arena16:00
TBAvTBAFisht Stadium20:00


Dk Mwakyembe Kufunga Tamasha la Karatu 2017

Na Mwandishi Wetu
KAMATI ya Olimpiki Tanzania (TOC) imemuomba Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe kuwa mgeni rasmi katika ufungaji wa tamasha la Michezo na Utamaduni la Karatu 2017.
Tamasha hilo ambalo hushindanisha michezo mbalimbali pamoja na ngoma za utamaduni na kwaya, litafikia kilele Desemba 23 katika viwanja vya Mazingira Bora mjini Karatu.

Mratibu wa tamasha hilo, Meta Petro amesema leo kwa njia ya simu kuwa,
wanatarajia Dk Mwakyembe ndiye atawafungia tamasha lao hilo, ambalo hufanyika kila mwaka.

Tamasha hilo ambalo huandaliwa na Filbert Bayi Foundation (FBF) kwa kushirikiana na TOC, Chama cha Riadha Karatu na kudhaminiwa na Olympic Solidarity,limekuwa chachu ya kuibua vipaji hasa vya riadha.

Petro anasema kuwa mbali na mbio za kilometa 10 na tano kwa wanaume na wanawake, pia kutakuwa na mbio za kilometa 2.5 kwa watoto, mbio za baiskeli za kilometa 60 kwa wanaume na wanawake kilometa 30, soka na mpira wa wavu.


Anasema kuwa mchezo wa soka na wavu fainali zake zitafanyika siku moja kabla ya kilele cha tamasha hilo, Desemba 22 na zawadi zao zitatolewa siku inayofuata, ambapo Dk Mwakyembe ndiye atakayekabidhi zawadi kwa washindi.

JKT Mbweni, Jeshi Hapatoshi Nusu Fainali Muungano

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
TIMU za netiboli za JKT Mbweni na Jeshi Stars zitakutana kesho katika moja ya mechi za nusu fainali za Ligi Kuu ya Muungano kwenye Uwanja wa Gymkhana.

Nusu fainali nyingine itawakutanisha mabingwa watetezi wa ligi hiyo ya Muungano Uhamiaji watakaocheza dhidi ya KVZ ya Zanzibar.

JKT Mbweni imefuzu kucheza nusu fainali baada ya kuongoza kundi lake la B na kufuatiwa na KVZ wakati Kundi A, Uhamiaji ndio wamemaliza washindi wa kwanza wakifuatiwa na Jeshi Stars.

Katika mechi za leo Ijumaa, JKT Mbweni iliibuka na ushindi wa mabao 41-36 dhidi ya JKT, ambapo washindi walikuwa mbele kwa 14-8, 29-18 na 34-29 katika robo ya kwanza hadi ya tatu.

Katika mchezo mwingine, Mafunzo iliibuka na ushindi wa mabao 48-41 dhidi ya Zima Moto, huku Mafunzo wakishinda 17-7, 26-20 na 38-30 katika robo zote.

KVZ waliifunga Polisi Arusha kwa mabao 53-46, ambapo washindi walitamba kwa 13-12, 29-21 na kufungwa 44-40 katika robo yatatu.


Katika mchezo mwingine, JKT Mbweni waliifunga Polisi Morogoro kwa mabao 56-25 huku washindi wakishinda kwa 13-3, 28-11 na 40-19 katika robo zote tatu.

Katika mashindano hayo, Tanzania Bara imeingiza timu tatu katika nusu fainali, ambazo ni mabingwa watezi Uhamiaji, mabingwa wa Tanzania Bara JKT Mbweni na Jeshi Stars wakati zanzibar imeingiza timu moja tu ya KVZ.

Wenger ahofia Mourinho kupaki basi kesho

LONDON, England
KOCHA Arsene Wenger hatarajii kabisa Jose Mourinho wa Manchester United kuegesha basi wakati watakapocheza na Arsenal leo kwenye Uwanja wa Emirates.

Timu hizo mbili zinakutana katika mchezo huo kila moja ikiwa imeshinda mechi tatu mfululizo za Lig Kuu, huku Man United ikiwa na pointi nne zaidi juu ya Arsenal klatika nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo.

United inaangalia kushinda ushindi wake wa kwanza katika majaribio nane dhidi ya wapinzani wake waliokatika bafasi sita za juu chini ya Mourinho,wakitoka sare mara tatu na kupoteza mara nne katika mechi saba zilizopita huku wakifunga mara moja tu.

Alipoulizwa kama anatarajia Mourinho atapaki basi, Wenger alijibu: "Hapana, Sitarajii kitu chochote maalum. Natarajia sisi kupambana na hali yoyote.

"Man Utd ni timu ngumu na ninatarajia sisi kuenda sambamba na matatizo yatakayotokea dhidi yetu. Watashambulia vizuri. Na sio kama watajilinda tu.

"Ni mchezo kati ya Arsenal na Man United nyumbani [the Emirates]. Ninachotaka ni kuelekeza nguvu katika mchezo huo na kuiandaa timu yangu vizuri, na kuipa timu yangu nafasi nzuri ya kushinda.

"Kwa sasa Man Utd inakwenda vizuri, na sisi tunafanya vizuri kwa sasa, hivyo utakuwa mchezo wenye ushindani wa hali ya juu.”

Mchezo huo umekuja katika kipindi kizuri katika msimu kwa Arsenal, kufuatia ushindi wa London derby dhidi ya Tottenham,na baadae dhidi ya Burnley na ule wa 5-0 Jumatano dhidi ya Huddersfield.

Hatahivyo, Wenger ana majeruhi kibao katika kikosi chake, pamoja na mshambuliaji Alexandre Lacazette aliyebadilishwa wakati wa mapumziko walipochea dhidi ya Huddersfield kutokana na maumivu ya nyomga.

Majeruhi mwingine ni Alexis Sanchez ambaye pia ilibidi kubadilisha baadae kutokana na kuhisi maumivu ya nyama za paja.


Wenger anatarajia Sanchez kuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo lakini tayari amekata tamaa na Lacazette, ikiwa na maana kuwa Olivier Giroud ataanza mchezo wa kwanza wa ligi kufuatia  ushindi wa mabao mawili dhidi ya Huddersfield.

Mwanzo Mwisho Ratiba Challenge Cup Kenya 2017

Desemba 3, 2017

Kundi A
Libya vs Tanzania
Kenya vs Rwanda

Desemba 4, 2017

Kundi B
Burundi vs Ethiopia

Desemba 5, 2017

Kundi A
Zanzibar vs Rwanda
Kenya vs Libya

Desemba 6, 2017

Kundi B
Uganda vs Burundi

Desemba 7, 2017

Tanzania vs Zanzibar
Rwanda vs Libya

Desemba 8, 2017

Kundi B
Sudan Kusini vs Ethiopia

Desemba 9, 2017

Kundi A
Rwanda vs Tanzania
Kenya vs Zanzibar

Desemba 10, 2017

Kundi B
 Sudan Kusini vs Burundi
Ethiopia vs Uganda

Desemba 11, 2017

Kundi A
Libya vs Zanzibar
Kenya vs Tanzania

Desemba 12, 2017

Kundi B
Uganda vs Sudan Kusini

Desemba 13, 2017

Mapumziko

Desemba 14, 2017

Nusu fainali 1 (Mshindi Kundi A vs Mshindi wa pili Kundi B)

Desemba 15, 2017

Nusu fainali 2 (Mshindi Kundi B vs Mshindi wa pili kundi A)

Desemba 16, 2017

Mapumziko

Desemba 17, 2017

Mshindi wa Tatu & Fainali



Bondia Anthony Joshua ataka umaarufu wa Federer

LONDON, England
NYOTA wa ndondi za uzito wa juu wa Uingereza, Anthony Joshua anataka kujijengea umaarufu katika ndondi za kulipwa kama ule wa Roger Federer katika mchezo wa tenisi.

Joshua hadi sasa ameshinda mapambano 20-0, yote yakiwa kwa KO na kumpatia umaarufu mkubwa katika mchezo huo.

Bondia huyo tayari ameweka rekodi ya kuingiza watazamaji wengi katika moja ya mapambano yake, likiwa limeingiza watazamaji 90,000 Aprili mwaka huu alipomsimamisha Wladimir Klitschko kwenye Uwanja wa Wembley hapa.

Baadae pambano lake jingine lililofanyika mwezi uliopita, liliingiza watazamaji 78,000, ambalo lenyewe alishinda kwa TKO dhidi ya bondia Carlos Takam lililofanyika kwenye Uwanja wa Manispaa wa Cardiff, Wales.

Kuna wataalamu wengi wanaamini kuwa bingwa huyo wa dunia wa WBA, IBF na IBO atakuwa mwiba mkali katika ngumi.

Federer, bingwa mara 19 wa mataji makubwa, anachukuliwa kwa kiasi kikubwa kuwa ni mcheza tenisi mkubwa zaidi katika kipindi chote na Joshua ana nia hiyo ya kujiweka katika nafasi hiyo.

"Sasa naelewa, natakiwa kucheza ndondi ikiwa nataka kujijengea jina, “alisema bondia huyo Muingereza mwenye umri wa miaka 28.

"Bado sijatekeleza jukumu langu. Lakini angalia bondia kama Muhammad Ali, ambaye amekuwa alama ya mchezo wa ndondi….”

"Ikiwa unataka kuwa watu kama hawa, unatakiwa kujibidiisha katika njia sahihi.

"Nataka kuwa kama akina [Cristiano] Ronaldos, [Lionel] Messis, Federers anayeshindana na [Rafael] Nadal, [Andy] Murray. Hilo nataka kulipeleka katika ngumu.”

CAF yazipiga nyundo SuperSport na TP Mazembe

CAIRO, Misri
BODI ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka la Afrika (Caf) limeziadhibu klabu za TP Mazeme na Supersport United baada ya mashabiki wao kuvamia uwanjani katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Jumamosi iliyopita.

Mchezo huo wa fainali uliofanyika Novemba 25 mwaka huu, ulipigwa kwenye Uwanja wa Lucas Moripe jijini Pretoria.

Kwa mujibu wa Ibara ya 83 na 151 ya Sheria za Caf, Supersport imepigwa faini ya dola za Marekani 15,000 kutokana na vurugu hizo za mashabiki.

Klabu hiyo ya Afrika Kusini pia imeonywa kutorudia kosa kama hilo, au watajikuta wakipewa adhabu ya kucheza bila mashabiki.

Kwa upande wa TP Mazembe, wenyewe wamepigwa faini ya dola za Marekani 5,000 kutokana na tabia za mashabiki wao, ambao walikiuka sheria namba 82 na 83 ya sheria za Caf.

Katika mchezo huo, TP Mazembe ya Congo ilifanikiwa kutetea taji lake iliyoshinda mwaka jana baada ya kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 2-1 baada ya kuilazimisha sare ya bila kufungana Supersport katika mchezo huo wa marudiano.


Katika mchezo wa kwanza, TP Mazembe ilitumia vizuri uwanja wake wa nyumbani na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Allardyce asaini miezi 18 kuifundisha Everton

LONDON, England
SAM Allardyce (pichani) anasema kuwa amekubali kuwa kocha mpya wa Everton baada ya kuingia mkataba wa miezi 18 wa kuifundisha timu hiyo.

Kocha huyo alisema kuwa ni ni jambo la aina yake kuwa kocha wa timu hiyo.

Allardyce anajiunga na klabu hiyo baada ya kurejea tena England juzi, kufuatia kuwa katika mapumziko mjini Dubai, kukamilisha makunaliano na bodi ya klabu ya Everton.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 63 alikuwa miongoni mwa watazamaji waliofika uwanjani kushuhudia Everton ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya West Ham kwenye Uwanja wa Goodison Park.

Mbali na Allardyce pamoja naye alikuwepo mmiliki Farhad Moshiri na mwenyekiti Bill Kenwright wakati timu yao ikitoa kichapo hicho kikubwa.

Sammy Lee anajiunga na klabu hiyo kama kocha msaidizi, wakati kocha wazamani wa Leicester Craig Shakespeare, ambaye alikuwa mtu wa karibu wa Allardyce wakati akiifundisha England kwa miezi minne, naye pi aataungana na benchi hilo la ufundi.

"Wakati wote nafikiri Everton ilikuwa klabu kubwa. Ni klabu kubwa kweli. Ni wazi, klabu imepitia katika hali ngumu na nina matumaini yote jayo tutaweka kando haraka na kuangali mengine.”


Mmiliki wa Everton Moshiri aliongeza: "Nimefurahi kumthibitisha Sam kuwa kocha wetu mpya. Uongozi imara utaleta ari na wachezaji wetu kufanya vizuri.”

Ally kuiongoza tena Uchukuzi Sports Club

Makamu Mwenyekiti  wa Klabu ya Uchukuzi, Bw. Hassan Ahmad akiwashukuru wapigakura kwa kutumia haki yao kuchagua viongozi wa klabu hiyo katika uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere. Nyuma waliosimama ni uongozi mpya wa klabu hiyo.
Na Mwandishi Wetu
MWENYEKITI aliyemaliza muda wake wa Klabu ya michezo ya Sekta ya Uchukuzi ,  Mohamed Ally ameshinda kwa kishindo kwa kutetea nafasi yake katika  uchaguzi wa klabu hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa Transit wa Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa (JNIA-TBI) kwa kupata kura 113.

Hatahivyo, Ally pamoja na kupigiwa kura nane (8) za hapana na sita (6) zikiharibika hakuwa na mpinzani baada ya aliyejitokeza awali Emmanuel  Tumaini kujitoa dakika chache kabla ya kuingia kwenye ukumbi wa mkutano wa uchaguzi.

Hassan Ahmad ameshinda nafasi ya Makamu Mwenyekiti kwa kupata kura 71 akiwashinda Hamis Mussa (57) na Neema Makassy (8); huku Katibu Mkuu akichaguliwa Mbura Tenga (73) aliyewashinda Katibu aliyemaliza muda wake Alex Temba (46), Ramadhani Kalima (5) na Leonard (2).

Mrisho Harambe ameweka rekodi kwa kushinda kwa kura 124 katika nafasi ya Katibu Msaidizi ambapo zikiwa ni kura nyingi zaidi walizopata wagombea wengine wa nafasi mbalimbali; na alimshinda Saidi Marusu aliyepata kura nane (8).

Mweka Hazina alichaguliwa Bw. Benjamin Bikulamti (87) aliyemshinda Wilson Magesa (42); huku wajumbe watano waliochaguliwa kutoka katika 14 walioomba kura ni Hilda Mwakatobe (75), Kurwa Sanga (72), Burton Willy (71), Evarist Mmanda (56) na Siraji Silimu (53).

Katibu aliyemaliza muda wake Bw. Alex Temba akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali mbele ya wapigakura wa klabu ya Uchukuzi kabla ya kufanyika uchaguzi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TB1). Aliyeshika chupa ya maji mbele ni Kocha Kenneth Mwaisabula ‘Mzazi’ akimsikiliza kwa makini.
Hatahivyo, Mwenyekiti wa uchaguzi huo Mputa Maokola amewataka viongozi wapya kudumisha ushirikiano baina yao na wachezaji, na endapo kumetokea matatizo wahakikishe wanasuluhisha ili kuepuka vurugu. 

Wasimamizi wengine kwenye uchaguzi huo ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE), Joseph Matiku kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) na Mapinduzi Ussi kutoka Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA).

  1. Wachezaji wa timu ya Uchukuzi wakihesabu kura za Katibu Mkuu mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Akiwashukuru wapigakura kwa niaba ya viongozi wenzake, Makamu Mwenyekiti, Ahmad amesema wanategemea mchango mkubwa wa mawazo kutoka kwa wanamichezo hao, na kuwataka wawakosoe endapo watakuwa wanakosea.

“Kwa niaba ya wenzangu tutajituma ili kufanikisha lengo letu la ushindi kwenye michezo mbalimbali tutakayoshiriki, lakini mtambue pia tunategemea mchango wenu wa mawazo katika kuendeleza klabu yetu ya Uchukuzi,” alisema Ahmad.


Mbura Tenga (mbele aliyesimama) akimwaga sera zake kwa wapigakura wa klabu ya Uchukuzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI).
Mbura Tenga (mbele aliyesimama) akimwaga sera zake kwa wapigakura wa klabu ya Uchukuzi uliofanyika kwenye ukumbi wa Jengo la Kwanza la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA-TBI).Hata hivyo, alisema sasa watatengeneza utaratibu wa kufanya wachezaji kukutana mara kwa mara katika michezo ya mabonanza na sio kusubiri michezo ya Mei Mosi na Shimiwi pekee ambayo inafanyika kila mwaka mara moja.